عن المِقدام بن معدي كرب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِذَا أَحَبَّ الرَّجُلُ أَخَاهُ فَلْيُخْبِرْهُ أَنَّهُ يُحِبُّهُ».
Imepokelewa Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Yakrib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapompenda mtu ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- moja ya sababu ambazo hutia nguvu mahusiano kati ya waumini na hueneza mapenzi baina yao, nako ni kuwa mtu atakapompenda ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda.
Mafunzo
Ubora wa mapenzi ya dhati yanayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa ajili ya masilahi ya kidunia.
Inapendeza na ni sunna kumueleza anayependwa kwa ajili ya Allah, ili kuongeza mapenzi na kuzoeana.
Kuenea kwa mapenzi baina ya waumini hutia nguvu udugu wa kiimani na huhifadhi jamii kuto pasuka na kufarakana.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 444) (5124).
سنن الترمذي (4/ 199) (2392).
السنن الكبرى للنسائي (9/ 87) (9963).
مسند أحمد (28/ 408) (17171).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 450).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص258).
رياض الصالحين للنووي، (ص138) (383).
سلسلة الأحاديث الصحيحة وشيء من فقهها وفوائدها، للألباني (1/ 777).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (1/ 247).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 279).
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alimsimulia akasema: Alinijia mwanamke mmoja akiwa na watoto wake wawili akiniomba, nikawa sikupata ndani kwangu zaidi ya tende moja, nikampatia, akaigawanya baina ya watoto wake, kisha akanyanyuka akatoka, muda si mrefu, akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsimulia kisa hicho, akasema: "Atakayesimamia chochote kwa watoto wa kike hawa, akawatendea wema, basi watakuwa ni kinga kwake kutokana na moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba mwanamke mmoja alimjia akiwa na mabinti zake wawili akimuomba chochote kinacholiwa, Aisha akawa hakupata kwake zaidi ya tende moja, akampatia basi mwanamke yule akaigawanya tende hiyo baina ya watoto wake, na yeye hakula chochote, kisha akanyanyuka na akaondoka, punde akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Aisha akamsimulia kisa hicho, akasema: Atakayesimamia chochote katika malezi ya mabinti hawa, akawatendea wema na akawalisha na akawanywesha na akawavisha, na akawa na subira juu ya hilo, basi watakuwa ni sitara na kinga kwake dhidi ya moto.
Mafunzo
Kuwalea watoto wa kike na kushughulika nao ni katika amali bora miogoni mwa amali njema zinazomuepusha mtu na moto.
Sunna ya kutoa chochote kilicho ndani ya uwezo wa mtu hata kama ni kidogo.
Huruma kubwa ya wazazi kwa watoto wao.
Kumebainishwa hali ya nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba riziki yake ilikuwa ya kumtosheleza pekee.
Kumebainishwa fadhila za kujinyima kwa ajili ya watu wengine, na kwamba hilo ni katika alama za waumini; kwani Aisha alimpendelea yule mwanamke na watoto wake kuliko nafsi yake, na hii inaonyesha juu ya ukarimu wake na moyo wake wa kujitolea pamoja na kuwa ana uvihitaji.
Zawadi ya watoto wa kike imeitwa kuwa ni mtihani; kwa sababu kuwalea kwake kuna shida na tabu nyingi, au kwa sababu ya baadhi ya watu kuwachukia, au ni kwa sababu mara nyingi wao huwa hawana vyanzo vya mapato ya maisha.
Uislamu ulikuja kung'oa mizizi ya desturi mbovu za zama za ujinga, na miongoni mwake nikuwa uliusia watu kuwalea vizuri watoto wa kike.
Mtu anapata malipo haya hata akiwa na binti mmoja kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 7) (5995).
صحيح مسلم (4/ 2027) (2629).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 353).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص199).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 151).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 106).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 277).
عن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «رَحِمَ اللهُ رَجُلًا سَمْحًا إِذَا بَاعَ، وَإِذَا اشْتَرَى، وَإِذَا اقْتَضَى».
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alimuombea rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila mwenye kuwa mwepesi mkarimu mpole katika biashara yake; Hamkadamizi mnunuzi katika bei yake, na anaamiliana naye kwa tabia njema, Mwepesi mkarimu mpole anaponunua; Hapunji na kupunguza thamani ya bidhaa, Mwepesi mkarimu mpole anapodai kulipwa madeni yake; hamtilii mkazo fukara na muhitaji, bali anamdai kwa upole na huruma, na anampa muda mwenye hali ngumu.
Mafunzo
Miongoni mwa malengo ya sheria ni kuhifadhi yenye kutengeneza mahusiano baina ya watu.
Himizo la kutumia tabia za hali ya juu katika miamala baina ya watu kuanzia kuuza na kununuwa na mfano wake.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 57) (2076).
نزهة المتقين (2/ 944).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 386).
منار القاري، لحمزة محمد قاسم (3/ 258).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 405).
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كان رجلٌ يُدَايِنُ الناسَ، فكان يقول لفتاه: إذا أتيتَ مُعسِرًا فتجاوز عنه، لعل اللهَ يَتجاوزُ عنا، فلقي اللهَ فتجاوز عنه».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuhusu bwana mmoja aliyekuwa akiamiliana na watu kwa mkopo, au akiwauzia kwa mkopo, Na alikuwa akisema kumwambia kijana wake aliyekuwa akikusanya madeni yaliyoko kwa watu: Utakapomwendea mdaiwa na akawa hana cha kulipa deni analodaiwa kwa sababu ya kushindwa "Basi, msamehe"; Ima kwa kumpa muda zaidi na kutong'ang'ania kumdai, Au kwa kukubali alichonacho hata kama kina mapungufu, na hiyo ni kwa hamu yake na tamaa yake ya kutaka Allah asimuadhibu na amsamehe, Alipofariki Allah akamsamehe na hakumuadhibu kwa makosa yake mengine.
Mafunzo
Wema katika kuamiliana na watu na kuwasamehe na kumpa uhuru mwenye hali ngumu ni katika sababu kubwa za mja kusalimika siku ya Kiyama.
Kuwafanyia wema viumbe na kutakasa matendo kwa ajili ya Allah na kutaraji katika rehema zake ni katika sababu za kupata msamha wa madhambi.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 176) (3480).
صحيح مسلم (3/ 1196) (1562).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 458).
التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (8/ 123).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 402).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري (5/ 1953).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (2/ 945).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu hatomsitiri ndugu yake katika jambo miongoni mwa mambo, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiyama; kwani malipo huendana na matendo, na stara ya Mwenyezi Mungu kwake inakuwa kwa kuzisitiri aibu zake na maasi yake kwa kutoyatangaza mbele ya umati wa siku ya Kiyama, na huenda inawezakuwa kwa kutoyahesabu na kutomkumbusha.
Mafunzo
Sheria ya kumsitiri muislamu anapofanya maasi, pamoja na kumkemea, na kumnasihi, na kumhofisha kwa Mwenyezi Mungu, ama akiwa ni katika watu wa shari na uovu wenye kutangaza wazi maasi na uovu, hawa haitakiwi kusitiriwa; kwa sababu kuwasitiri kunawapa ujasiri wa kufanya maasi, bali wanatakiwa kushitakiwa katika mamlaka husika, hata kama watatajwa kwa majina; kwa sababu mtu anakuwa katangaza wazi yeye mwenyewe maovu yake na maasi yake.
Himizo la kusitiri aibu za watu wengine.
Miongoni mwa faida za kusitiri: Ni kumpa fursa mkosefu ya kuirejea nafsi yake na atubie kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu kutangaza aibu na fedhehe ni katika kueneza maovu, na kunaharibu hali ya hewa ya jamii, na kunawahadaa watu kuendelea kuyatenda.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2002) (2590).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 329).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 255).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 533).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 14).
Kutoka kwa Abuu Dharri, Jundubi bin Junada, na Abuu Abdulrahman, Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yao kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaAmesema Al-tirmidhiy: Hadithi hii ni Hasan
Maelezo
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo matatu: La kwanza: Kumuogopa Mwenyezi Mungu na hii inakuwa kwa kutekeleza wajibu, na kuacha maharamisho, katika kila mahali na nyakati na hali, katika siri na wazi, na wakati wa afya na balaa na mengineyo. La pili: Ukiangukia katika ovu, basi fanya baada yake jambo jema kama swala na sadaka na wema na kuunga udugu na toba na mengineyo, kwani hayo hufuta madhambi. La tatu: Ishi na watu kwa tabia njema, kama kutabasamu katika nyuso zao, na upole na ulaini na kutenda wema na kuacha maudhi.
Mafunzo
Fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kwa kuwahurumia na kuwasamehe na kuwafutia makosa.
Hadithi imekusanya haki tatu: Haki ya Mwenyezi Mungu ya kuogopwa, na haki ya nafsi kwa kufanya mema baada ya mabaya, na haki ya watu wengine kwa kuishi nao kwa tabia njema.
Himizo la kufanya mema baada ya maovu na kuwa na tabia njema ni miongoni mwa sehemu ya uchamungu, isipokuwa alitaja peke yake kwa sababu ya haja ya kuliweka wazi.
Marejeo
الأربعون النووية (ص100) (ح18).
سنن الترمذي (3/ 526) (1987).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص40).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص195).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، لعبد المحسن البدر (ص67).
Kutoka kwa Nawwasi bin Samaan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema: "Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia watu wasilione".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema:
Kubwa kabisa katika wema ni tabia njema pamoja na Allah, kwa kumcha, na pamoja na watu, kwa kuvumilia kero, na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na kuunga udugu na kutii na kuwa mpole na kutenda wema, na kuishi vizuri na familia, na kusuhubiana na watu vizuri.
Na ama dhambi ni kila kitakachokereketa ndani ya nafsi katika mambo yenye kutatiza, na kifua kikakosa utulivu na kutokunjuka, na moyo ukapata shaka, na ukaogoga kwa sababu ni dhambi, na ukawa hukutaka kulidhihirisha kwa mtu au hadharani mbele za watu kwakuwa ni baya, na hii ni kwa sababu nafsi hupenda watu waone yale mazuri yake, ikiwa itachukia watu kuyaona baadhi matendo yake basi hayo ndiyo madhambi wala hayana kheri ndani yake.
Mafunzo
Himizo la kuwa na tabia njema; kwa sababu tabia njema ni katika mambo makubwa ya wema.
Haki na batili haviwezi kumchanganya muumini, bali anaijua haki kwa nuru aliyonayo ndani ya moyo wake, na anaichukia batili na kuikataa.
Miongoni mwa alama za dhambi ni moyo kukosa utulivu na kuwa na shaka, na kuchukia watu wasilione.
Amesema As-Sanadi: Hii ni katika mambo yenye kutatiza ambayo watu hawajui kutofautisha moja kati ya pande mbili; na kama si hivyo basi kilichoamrishwa na sheria pasina kuonekana dalili ndani yake ni kinyume na hilo katika wema, na yaliyokatazwa hivyo hivyo miongoni mwa madhambi, na hayo hakuna haja ya kuuliza ama kuutazama moyo na kuona utulivu wake.
Wanaosemeshwa katika hadithi hii ni wale wenye maumbile salama (ambao mioyo yao na akili zao hazijavurugwa na fikra potofu), na si wenye mioyo iliyofunikwa isiyojua jema wala kulikataa ovu isipokuwa yale iliyonyweshwa katika matamanio yake.
Amesema Attwayibi: Inasemekana: Imefasiriwa maana ya wema katika hadithi kwa maana nyingi, akaifasiri katika baadhi ya sehemu kuwa ni yale ambayo nafsi imetulizana kwayo na moyo ukatuliza pia, na akaifasiri katika sehemu nyingine kuwa ni imani, na katika sehemu nyingine, kwa yale yanayokuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na hapa ameifasiri kwa kuwa na tabia njema, na akafasiri tabia njema kuwa: Ni kuvumilia maudhi na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na yote hayo yanakaribiana katika maana.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1980) (2553).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية التحفة الربانية (ص62).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص267).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للنووي وابن رجب رحمهما الله (ص92).
عن شداد بن أوس رضي الله عنه قال: ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja.
Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa.
Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.
Mafunzo
Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1548) (1955).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص38).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص185).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص65).
فتح الباري، لابن حجر (9/ 644).
شرح النووي على مسلم (13/ 107).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com