Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.
- Kumebainishwa tabia alizokuwa nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, tabia za juu na kuwa kwake mbali na tabia mbaya.
- Himizo la kufanya tabia njema na kujiweka mbali na tabia mbaya.
- Kumekemewa kujilazimisha machafu katika kauli na maneno machafu.
- Kumekemewa kunyanyua sauti juu ya watu na kuwapigia makelele.
- Himizo la kuukabili ubaya kwa wema, na kusamehe na kufuta kosa.
سنن الترمذي (3/ 543) (2016). مسند أحمد (42/ 256) (25417). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر(6/ 575). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، القسطلاني (9/ 30). معجم اللغة العربية المعاصرة (2/ 1629). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (9/ 3717).