Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «المُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ، وَالمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo
  1. Ukamilifu wa Uislamu hauwi isipokuwa kwa kutofanyia maudhi watu wengine, kwa vitendo au kwa hila yoyote.
  2. Ametaja ulimi na mkono pekee pasina viungo vingine; kwa sababu ya wingi wa makosa yake na madhara yake, kwani shari nyingi hutokea kupitia viwili hivi.
  3. Himizo la kuacha maasi na kushikamana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Muislamu bora kuliko wote ni yule mwenye kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waislamu.
  5. Uadui unaweza kuwa kwa kauli au kitendo.
  6. Kuhama kuliko kamilika ni kuyahama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 11) (10). صحيح مسلم (1/ 65) (40). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 236). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 511). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 306).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kuzidi kwa Imani na Kupungua kwake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com