Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa kunakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa, atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ndio muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake basi naye ni muumini, na atakayepigana nao kwa ulimi wake basi naye ni muumini, na hakuna zaidi ya hapo katika imani punje ndogo ya Haradali" (yaani kwa asiyefanya hivyo hana imani hata punje ndogo).
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa umma kabla yake isipokuwa huwa na watu safi na watetezi, na mujahidina wa kweli kutoka katika umma wake wanaofaa kwa ukhalifa (uongozi) baada yake, wanaofuata Sunna zake na kufuata amri yake, kisha baada ya hao watangulizi wema wanakuja watu ambao hawana kheri ndani yake; Wanasema wasiyoyafanya, na wanafanya yale ambayo hawakuamrishwa kuyafanya, na atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ni Muumini, atakayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumini, na hakuna imani hata chembe ya haradali (ulezi) baada yake.
Mafunzo
Himizo la kupambana na wanaokwenda kinyume na sheria kwa kauli zao na vitendo vyao.
Moyo kutokukemea uovu ni dalili ya udhaifu wa imani au kutoweka kwake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwafanyia wepesi Manabii kuwapata wenye kubeba ujumbe wao baada yao.
Atakayetaka kusalimika basi anatakiwa kufuata njia ya Manabii; kwa sababu kila njia isiyokuwa njia yao ni maangamivu na upotovu.
Kila zama zinavyozidi kuwa mbali na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Masahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao watu huzidi kuacha mafundisho na kufuata matamanio na kuzusha mambo ya uzushi.
Kumebainishwa daraja za Jihadi, nakuwa ni kwa mkono kwa mwenye kuweza kuuondoa uovu, kama wasimamizi na viongozi na watawala, na kwa kauli inakuwa kwa kubainisha haki na kuwalingania watu, na kwa moyo inakuwa kwa kuukemea uovu na kutoupenda au kuuridhia.
Ulazima wa kuamrisha mema na kukataza uovu.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 69) (50).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 276).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص148).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 16).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 209).
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الْإِيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ -أَوْ بِضْعٌ وَسِتُّونَ- شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الْأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الْإِيمَانِ».
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani, na haya ni sehemu katika imani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa imani ina sehemu moja pamoja na mambo mengi, yanakusanya matendo itikadi na kauli.
Nakuwa jambo la juu zaidi katika mambo ya imani ni kauli ya: Laa ilaaha illa llaah", kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi matakwa yake, yakuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi Mmoja wa pekee mwenye kustahaki kuabudiwa peke yake pasina mwingine zaidi yake.
Nakuwa tendo dogo kabisa katika matendo ya imani ni kila chenye kuwaudhi watu katika njia zao.
Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa haya ni katika mambo ya imani, nayo ni tabia inayomsukuma mtu kufanya mazuri na kuacha mabaya.
Mafunzo
Imani inadaraja baadhi yake ni bora kuliko zingine.
Imani ni kauli na matendo na itikadi.
Kumuonea haya Allah Mtukufu hupelekea: Kuwa asikuone pale alipokukataza, na asikukose pale alipokuamrisha.
Kutajwa idadi hakumaanishi kuishia hapo, bali inamaanisha wingi wa matendo ya imani, kwani waarabu wanaweza kutaja idadi ya kitu na wasimaanishe kukanusha idadi nyingine isiyokuwa hiyo.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 11) (9).
صحيح مسلم (1/ 63) (35).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 154).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 169).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص106).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم لهلالي (1/ 205).
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mafunzo
Ukamilifu wa Uislamu hauwi isipokuwa kwa kutofanyia maudhi watu wengine, kwa vitendo au kwa hila yoyote.
Ametaja ulimi na mkono pekee pasina viungo vingine; kwa sababu ya wingi wa makosa yake na madhara yake, kwani shari nyingi hutokea kupitia viwili hivi.
Himizo la kuacha maasi na kushikamana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Muislamu bora kuliko wote ni yule mwenye kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waislamu.
Uadui unaweza kuwa kwa kauli au kitendo.
Kuhama kuliko kamilika ni kuyahama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 11) (10).
صحيح مسلم (1/ 65) (40).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 236).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 511).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 306).
عن أبي سعيد الخُدْريِّ رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ».
Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anatuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kuuondoa uovu, na uovu ni kila alilolikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kadiri ya uwezo, Hivyo basi ikiwa mtu atauona uovu basi ni wajibu juu yake kuuondosha kwa mkono wake ikiwa atakuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo. Ikiwa atashindwa kuondosha uovu kwa mkono wake basi na auondoshe kwa ulimi wake, kwa kumkataza mwenye kufanya uovu huo, na amueleze madhara ya uovu huo na amuongoze katika kheri badala ya kufanya shari hiyo. Basi ikiwa atashindwa hatua hii ya pili, basi auondoshe uovu kwa kuchukia moyoni mwake, kwa kuuchukia uovu huo, na aazimie moyoni mwake kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo angeuondosha, Na kuuondosha uovu kwa moyo ni katika kiwango dhaifu zaidi cha imani katika kuuondosha uovu
Mafunzo
Miongoni mwa faida za hadithi hii ni kuwa hadithi hii ni msingi katika kuweka wazi hatua na taratibu za kuuondoa uovu.
Maamrisho ya kwenda hatua kwa hatua katika kukataza uovu, hatua zote hizo ni kwa mujibu wa uwezo wa mtu.
Kukataza uovu katika dini ni mlango mpana sana suala hilo hakuna wakulikwepa, na hulazimishwa kila muislamu kufanya hivyo kwa kadiri ya uwezo wake.
Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni katika mambo yanayofungamana na imani, na imani kwa kawaida huzidi na kupungua.
Ni sharti katika kukataza uovu: kuwa na elimu ya kuwa kitendo hicho ni uovu.
Ni sharti katika kuondoa uovu: Usipelekee kutokea uovu mkubwa kuliko huo.
Kukataza uovu kuna taratibu zake na masharti ambayo anapaswa muislamu kujifunza.
Kukataza maovu kunahitajia siasa ya kisheria, na kuwa na ujuzi na elimu.
Kutokuondosha uovu kwa moyo ni dalili ya udhaifu wa imani.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 69).
جامع العلوم والحكم (2/245).
المعين على تفهم الأربعين (ص 393).
شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 336).
البحر المحيط الثجاج (2/204).
فتح القوي المتين للعباد (ص 116).
Imepokelewa hadithi kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, amesema: Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi tutaadhibiwa kwa tuliyoyafanya katika zama za ujinga kabla yakuwa waislamu?Akasema "Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anatuwekea wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuingia katika Uislamu, Na kuwa mwenye kusilimu na uislamu wake ukawa mzuri na akawa mtakasifu na mkweli, basi hatoadhibiwa kwa makosa aliyoyafanya kabla ya uislamu, Na atakaye fanya uovu akiwa katika uislamu, yaani kwa kuwa mnafiki au akatoka katika dini yake, basi huyo ataadhibiwa kwa aliyoyafanya akiwa bado hajaingia katika uislamu na ataadhibiwa pia kwa yale aliyoyafanya akiwa katika uislamu.
Mafunzo
Maswahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutilia umuhimu mambo mazito, na hofu yao kwa yale yaliyokuwa kabla ya Uislamu.
Mahimizo ya kudumu kwenye Uislamu.
Ubora na fadhila za kuingia katika uislamu, na kuingia katika uislamu hufuta matendo mabaya yaliyopita.
Mwenye kutoka katika uislamu na mnafiki, atahukumiwa kwa kila kitendo alichokifanya kabla ya kusilimu kwake, na kuhukumiwa kwa dhambi alilofanya kwenye uislamu.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 14) (6921).
صحيح مسلم (1/ 111) (120).
مشارق الأنوار على صحاح الآثار (2/229).
الكواكب الدراري (24/43).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (24/ 76).
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi wakamuuliza: kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Lilikuja kundi la maswahaba kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na wakamuuliza kuhusiana na yanayowatokea katika nafsi zao miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanakuwa kwao ni mazito kuyasema kutokana na ubaya wake na kupenda kwao kujiepusha nayo Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: kwa hakika hiki ambacho mnakipata kwenye nafsi zenu ndiyo imani ya kweli na uhakika ambao unawapa msukumo ili kuzuia anayoyaweka shetani katika nyoyo na kuwazuieni kuyasema na kuyaona ni mazito kwenye nafsi zenu, na shetani kutoweza kuimiliki mioyo yenu, tofauti na yule ambaye ametawaliwa na shetani kwenye moyo wake akashindwa kupata chenye kumzuia kusema .
Mafunzo
Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, pale ambapo shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
Kutokubali na kusadikisha kinachotakwa na nafsi miongoni mwa wasiwasi, kwani wasiwasi hutokana na shetani.
Wasiwasi wa Shetani haumdhuru muumini, lakini anatakiwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na wasiwasi wake, na aache kuendekeza wasiwasi.
Haipasi kwa muislamu kunyamazia mambo yenye kumtatiza miongoni mwa mambo yanayo husu dini yake, na anapasa kuuliza kuhusu hilo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 119) (132)، معالم السنن (4/174)، المفهم للقرطبي (1/344)، شرح النووي على مسلم (2/154)، البحر المحيط الثجاج (3/622).
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Umar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu."
Imepokelewa na Hakim na TabaraniDarajaSahihi
Maelezo
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Imani huoza katika moyo wa muislamu na inachakaa kama inavyochakaa nguo mpya kwa kutumika muda mrefu; Na kuoza huko ni kwa sababu ya udhaifu katika ibada, au kwa sababu ya kufanya maasi na kuzama kwenye matamanio. Basi anatoa muongozo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tumuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu azifanye kuwa mpya imani zetu, kwa kutekeleza mambo ya wajibu na kuzidisha kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha.
Mafunzo
Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu uimara na kuzifanya kuwa mpya imani katika nyoyo.
Imani sahihi ni kauli matendo na itikadi, na imani inazidi kwa kutii, na hupungua kwa kufanya maasi.
Marejeo
المستدرك على الصحيحين للحاكم (1/ 45) (5)، المعجم الكبير للطبراني (13/ 36) (84)، النهاية في غريب الحديث والأثر، ص(282)، النهاية (1/316)، فيض القدير (2/323)، التنوير شرح الجامع الصغير (3/434).
Kutoka kwa Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini mkweli katika imani yake uliyetulizana moyo wake kwa imani yake, atapata ukunjufu na wasaa na furaha ndani ya moyo wake na utam na ladha ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu endapo ataridhia kwa mambo haya matatu:
La kwanza: Akiridhika kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wake Mlezi, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayomfikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa muktadha wa ulezi, ikiwemo kugawa riziki na hali za waja, asipate upinzani kwa kitu chochote ndani ya nafsi yake, na asitafute Mola Mlezi zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
La pili: Aridhie kuwa Uislamu ndio Dini ya kweli, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayofungamana na Uislamu kama sheria na wajibu, na asipite njia nyingine isiyokuwa Uislamu.
La tatu: Aridhie kuwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake na afurahie yote aliyokuja nayo pasina kusitasita wala kutia shaka, na asipite ila njia inayokwenda sambamba na muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake.
Mafunzo
Imani ina utamu na ladha inayoonjwa kwa mioyo, kama inavyoonjwa ladha ya chakula na kinywaji kwa mdomo.
Mwili haupati ladha ya chakula na kinywaji isipokuwa unapokuwa na afya njema, hivyo hivyo hata moyo ukisalimika na maradhi ya matamanio potofu, na matamanio yaliyoharamishwa, utapata utamu wa imani, na utakapougua na nakuwa mgonjwa kamwe hauwezi kupata utamu wa imani, bali unaweza kupata utamu wa mambo yanayoangamiza kama matamanio na maasi.
Mwanadam atakaporidhia jambo na akaliona kuwa zuri linakuwa jepesi kulifanyia kazi, na wala hakuna kitakachoweza kumpa tabu katika hilo, na atafurahia kwa kila kilichokuja katika jambo hilo, na bashasha itaingia ndani ya moyo wake, hivyo hivyo hata muumini imani inapoingia ndani ya moyo wake, huwa rahisi kwake kumtii Mola wake Mlezi na nafsi yake huhisi ladha, na hakuna tabu zitakazomuwia ugumu.
Amesema Ibnil Qayyim: Hadithi hii imekusanya kuridhia uumbaji na upangiliaji wake Mtukufu na uungu wake, na kuridhika na Mtume wake na kumtii, na kuridhika na dini yake na kujisalimisha kwa dini hiyo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 62) (34)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 11)، إكمال المعلم بفوائد مسلم (1/ 270).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com