Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Majina na Hukumu.

Hadithi 69

Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini

عن بعض أزواج النبي صلى الله عليه وسلم عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً».
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatahadharisha Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kuwaendea wapiga ramli na hili ni jina la kiujumla la kuhani na mtabiri wa nyota na mpiga ramli na mfano wao, katika wale wanaotumia ishara za vitanguliza ili kudai kujua elimu ya ghaibu, nakuwa kumuuliza pekee mambo ya ghaibu Mwenyezi Mungu atamnyima thawabu za swala yake siku arobaini; na hiyo ni adhabu kwake kwa kosa hili na dhambi kubwa.

Mafunzo
  1. Uharamu wa ukuhani, na kwenda kwa makuhani na kuwauliza mambo ya ghaibu.
  2. Mtu anaweza kunyimwa thawabu za ibada ikiwa ni adhabu kwake kwa kutenda kwake maasi.
  3. Yanaingia katika hadithi hii yanayoitwa nyota na kutazamia, na kusoma viganja na vikombe hata kama ni kwa kutaka kujua pekee; kwa sababu hiyo yote ni katika ukuhani na ni katika kudai kujua elimu ya ghaibu.
  4. Ikiwa haya ndiyo malipo ya mwenye kumuendea mpiga ramli, ni vipi malipo ya mpiga ramli mwenyewe?.
  5. Swala za siku arobaini zinaangukia katika kutokubalika, si wajibu kuzilipa lakini hazina thawabu ndani yake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1751) (2230). مسند أحمد (27/ 197) (16638). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص238). الملخص في شرح كتاب التوحيد، للفوزان (ص213).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu

عن جابر رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَرَأَيْتَ إِذَا صَلَّيْتُ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ، وَصُمْتُ رَمَضَانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلَالَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ؟ قَالَ: «نَعَمْ»، قَالَ: وَاللهِ لَا أَزِيدُ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا.
Hadithi imepokelewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo", Akasema mtu yule: "Namuapia Mwenyezi Mungu sizidishi zaidi ya matendo hayo kitu chochote".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.

Mafunzo
  1. Muislamu kupupia juu ya kufanya mambo yaliyo faradhishwa na kuacha yaliyoharamishwa, na yawe malengo yake ni kuingia peponi.
  2. Umuhimu wa kufanya yaliyo halali na kuamini uhalali wake, na kuharamisha yaliyo haramu na kuamini uharamu wake.
  3. Kufanya yaliyo wajibu na kuacha yaliyo haramu ni sababu za kuingia Peponi.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 44) (15). جامع العلوم والحكم (1/513). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 215). فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 77).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com