عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَدَاةَ الْعَقَبَةِ وَهُوَ عَلَى نَاقَتِهِ: «الْقُطْ لِي حَصًى» فَلَقَطْتُ لَهُ سَبْعَ حَصَيَاتٍ، هُنَّ حَصَى الْخَذْفِ، فَجَعَلَ يَنْفُضُهُنَّ فِي كَفِّهِ وَيَقُولُ: «أَمْثَالَ هَؤُلَاءِ فَارْمُوا» ثُمَّ قَالَ: «أَيُّهَا النَّاسُ، إِيَّاكُمْ وَالْغُلُوَّ فِي الدِّينِ، فَإِنَّما أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ الْغُلُوُّ فِي الدِّينِ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake asubuhi ya tukio la Akaba huku akiwa juu ya Ngamia wake: "Niokotee kijiwe" Nikamuokotea vijiwe saba, navyo ni vijiwe vya kurusha wakati wa kuwinda, akawa akivipuliza katika kiganja chake huku akisema: "Mfano wa vijiwe hivi basi rusheni" Kisha akasema: "Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini".
Imepokelewa na Ibn Majah, Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake yakuwa alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya kuchinja (Siku ya Idd kubwa) asubuhi ya kurusha vijiwe (kwa walioko Makka katika ibada ya Hija) katika Hija ya kuaga, Akamuamrisha amuokotee vijiwe vya kurusha, akamuokotea vijiwe saba, kimoja miongoni mwake kina saizi ya kijiwe cha kuwindia, akaviweka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkononi mwake kisha akavitikisa, na akasema: Kwa vijiwe vya mfano kama huu basi rusheni, Kisha akatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuchupa mipaka na kujilazimisha na kuvuka kiasi katika mambo ya dini, kwani kilichowaangamiza umma waliotangulia ni kuvuka mipaka na kujiwekea mkazo katika dini.
Mafunzo
- Katazo la kuchupa mipaka katika dini, na kumeelezwa ubaya wa mwisho wake, nakuwa hilo ni sababu ya kuangamia.
- Kuchukua mazingatio kwa Umma zilizopita ili kuyaepuka makosa waliyotumbukia ndani yake.
- Himizo la kuiga kutoka katika Sunna.
Marejeo
سنن النسائي (5/ 268)(3057).
سنن ابن ماجه (4/ 228) (3029).
مسند أحمد (5/ 298) (3248).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص165).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص179).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم سئل عن النُّشْرَةِ؟ فقال: هي من عمل الشيطان.
Kutoka kwa Jaabir radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.
Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Nikuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake - Aliulizwa kuhusu kumtibu aliyerogwa kwa njia ambayo walikuwa wakiijua tangu zama za ujinga, mfano: kuondoa uchawi kwa uchawi ni ipi hukumu ya hilo, akajibu rehema na Amani zimfikie kuwa hiyo ni katika kazi za shetani, au hufanyika kupitia yeye; kwasababu inakuwa kwa aina ya uchawi na kwa kuwatumia mashetani, hiyo ni ushirikina na ni haramu. na ama kutibu uchawi kunakofaa: ni kuufungua uchawi kwa kisomo cha ruqya au kuutafuta, na kuufungua kwa mkono pamoja na kusoma Qur'ani au kwa dawa za halali.
Mafunzo
- Sheria ya kuwauliza wanachuoni katika yale yanayotatiza hukumu yake; kwa tahadhari ya kutoangukia katika haramu.
- Katazo la kutibu uchawi kwa namna wanayoifahamu watu wa zama za ujinga; kwasababu ni uchawi na uchawi ni ukafiri.
- Nikuwa kazi za shetani zote zimeharamishwa.
Marejeo
1- الملخص في شرح كتاب التوحيد، صالح بن فوزان بن عبد الله الفوزان، دار العاصمة، الرياض، الطبعة: الأولى، 1422هـ - 2001م.
2- الجديد في شرح كتاب التوحيد، محمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي، تحقيق: محمد بن أحمد سيد، مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م.
3- سنن أبي داود، سليمان بن الأشعث أبوداود، تحقيق: محمد محيي الدين عبد الحميد، المكتبة العصرية، صيدا، بيروت.
4- مسند الإمام أحمد بن حنبل، أحمد بن حنبل أبو عبدالله الشيباني، تحقيق: شعيب الأرنؤوط و عادل مرشد، وآخرون، تحت إشراف: عبد الله بن عبد المحسن التركي، مؤسسة الرسالة، الطبعة: الأولى، 1421هـ - 2001م.
5- سلسلة الأحاديث الصحيحة وشيء من فقهها وفوائدها، محمد ناصر الدين الألباني، مكتبة المعارف للنشر والتوزيع، الرياض.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ عَدْوَى وَلاَ طِيَرَةَ، وَلاَ هَامَةَ وَلاَ صَفَرَ، وَفِرَّ مِنَ المَجْذُومِ كَمَا تَفِرُّ مِنَ الأَسَدِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza baadhi ya mambo ya zama za kabla ya Uislamu, kuwa kama ni onyo dhidi yao, na kwa kuwabainishia kuwa amri yote iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna kinachotokea isipokuwa kwa amri yake, na kadari zake, nayo ni:
La kwanza: Watu wa zama za kabla ya Uislamu waliamini kwamba ugonjwa huwa unaambukiza peke yake. Kwa hiyo, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akakataza kuamini kwamba ugonjwa huwa una asili ya kuambukiza kutoka kwa mgonjwa kwenda mgonjwa mwingine. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kuundesha ulimwengu; Na Yeye ndiye anayeteremsha maradhi na kuyaondoa, na halitokei hilo ila kwa kutaka kwake na kwa Kadari Yake.
La Pili: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakitoka kwa ajili ya safari au biashara walikuwa wanawafukuza ndege, wakiruka kwenda kulia wanafurahi, na wakiruka kushoto wanakata tamaa na kurudi (wakiamini kuwa ni mkosi) basi, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akakataza hali hii ya kuamini mikosi kwa sababu ya ndege, na akabainisha kuwa ni imani potofu.
Tatu: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakisema: Ndege bundi akitua juu ya nyumba, kuna msiba utawapata watu wa nyumba hiyo. Kwa hivyo, akakataza rehema na amani ziwe juu yake, kuamini mikosi katika hilo.
Nne: Ni haramu kuamini mwezi wa Swafari kuwa ni mikosi, ambao ni mwezi wa pili katika miezi ya mwandamo. Ilisemekana kuwa Swafari ni: Nyoka tumboni anayeambukiza mifugo na watu, wanadai kuwa anaambukiza zaidi ya upele; akakanusha imani hii.
Tano: Aliamrisha kujitenga mbali na mwenye ugonjwa wa ukoma kama vile mtu anavyojiweka mbali na simba. Hii ni kujikinga na kutafuta usalama kwa ajili yake na kufanya sababu alizoamrisha Mwenyezi Mungu, na ukoma ni maradhi ambayo viungo vya mtu hulika.
Mafunzo
- Umuhimu wa kumwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kufanya sababu za kisheria.
- Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari ya Mwenyezi Mungu, na kwamba sababu ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na Yeye ndiye anayezifanya zitokee au kuondoa athari zake.
- Kubatilika kwa baadhi ya mambo wanayoyafanya baadhi ya watu kwa kupima bao kwa kutumia rangi, kama vile nyeusi na nyekundu, au namba fulani, na majina, na watu wenye ulemavu.
- Katika kukataza ukaribu na wenye ukoma na wale walio na magonjwa ya kuambukiza; Ni moja ya sababu ambazo Mwenyezi Mungu aliweka desturi kuwa zinapelekea katika matokeo yake. Sababu hazijitegemei zenyewe binafsi, bali ni Mwenyeezi Mungu ambaye, Akitaka, Anaziondoa nguvu zake, kwa hivyo haziwezi kuathiri chochote, na Akitaka, Anazibakisha, hivyo zitaweza kuathiri.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 126) (5707).
صحيح مسلم (4/ 1742) (2220).
فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (ص307).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 565).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص228).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص253).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص77).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَطَمَ الخُدُودَ، وَشَقَّ الجُيُوبَ، وَدَعَا بِدَعْوَى الجَاهِلِيَّةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amekataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na akatahadharisha kuhusu baadhi ya vitendo vya watu zama za ujinga akasema: Si miongoni mwetu:
La kwanza: Atakayepiga mashavu, na ametaja mashavu pekee kwa sababu ndio watu hufanya mara nyingi katika hilo, na vinginevyo kupiga sehemu zingine kunaingia ndani uso.
La pili: Kuchana uwazi wa nguo ili aingize kichwa kwa sababu ya huzuni kubwa.
La tatu: Akaomboleza kwa maombolezo ya za zama za ujinga kama kujiombea maangamivu na laana, na malalamiko, na makelele na mengineyo.
Mafunzo
- Kemeo lililokuja katika hadithi hii linaonyesha kuwa matendo haya yote ni katika madhambi makubwa.
- Ulazima wa kuwa na subira katika msiba, na uharamu wa kuchukizwa na kadari za Mwenyezi Mungu zenye kuumiza, na kulidhihirisha hilo: Kwa kulia kwa malalamiko au makelele au kunyoa, au kuchana nguo au mengineyo.
- Uharamu wa kuwaiga watu wajinga kwa mambo yao ambayo sheria imeyathibitisha kwao.
- Hakuna tatizo kuhuzunika na kulia, kwani hili halipingani na subira juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ni huruma aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika nyoyo za ndugu wa karibu na vipenzi.
- Ni lazima kwa muislamu kuridhia maamuzi ya Mwenyezi Mungu, na asiporidhia basi kusubiri ni wajibu.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 81) (1294).
صحيح مسلم (1/ 99) (103).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص287).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 379) .
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عمران بن حصين رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ تَطَيَّرَ أَوْ تُطُيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ، وَمَنْ عَقَدَ عُقْدَةً، وَمَنْ أَتَى كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ».
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
Imepokelewa na AlbazzarDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Katoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mwayo:
La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo.
La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake.
La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.
Mafunzo
- Uwajibu wa kumtegemea Allah na kuamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, na kuharamishwa kwa imani za mikosi na nuksi na uchawi na ukuhani, au kuwauliza wenye mambo hayo.
- Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
- Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.
Marejeo
مسند البزار = البحر الزخار (9/ 52) (3578).
شرح السنة للبغوي (12/ 182).
مجموع الفتاوى (35/ 173).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 543).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص315).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص242).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص217).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عائشة رضي الله عنها قالت: سَأَلَ أُنَاسٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْكُهَّانِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسُوا بِشَيْءٍ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، فَإِنَّهُمْ يُحَدِّثُونَ أَحْيَانًا بِالشَّيْءِ يَكُونُ حَقًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تِلْكَ الْكَلِمَةُ مِنَ الْحَقِّ يَخْطَفُهَا الْجِنِّيُّ فَيَقُرُّهَا فِي أُذُنِ وَلِيِّهِ قَرَّ الدَّجَاجَةِ، فَيَخْلِطُونَ فِيهَا أَكْثَرَ مِنْ مِائَةِ كَذْبَةٍ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kuna watu walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu makuhani, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawana lolote" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wao husimulia jambo baadhi ya nyakati na likawa kweli, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wale wanaoeleza mambo yajayo yaliyofichikana, akasema: Msiwajali, na wala msiyachukue maneno yao, na wala msiyajali mambo yao.
Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao.
Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).
Mafunzo
- Katazo la kuwasadikisha makuhani, nakuwa wanayoyasema ni uongo na uzushi, hata kama watasema ukweli katika baadhi ya nyakati.
- Mbingu zimehifadhiwa dhidi ya Mashetani kwa kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili wasije kusikiliza chochote katika wahyi au kinginecho, isipokuwa atakayeiba kusikiliza na akasalimika na kupigwa kimondo.
- Majini hujifanyia vipenzi katika binadamu.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 47) (6213).
صحيح مسلم (4/ 1750) (2228).
نزهة المتقين (2/ 1143).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 557).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 177).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (7/ 2904).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 404).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com