Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vitenguzi vya uislamu.

Hadithi 6

Hauondoi uchawi ila mchawi

ورُوي عن الحسن أنه قال: "لا يحل السحر إلا ساحر".
Na imepokelewa kutoka kwa Hassan yakwamba yeye amesema: "Hauondoi uchawi ila mchawi".
Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah - Imepokelewa na AlkhatwabyDarajaNi nzuri
Maelezo

Nushra, ni kuondoa uchawi, na uwazi wa maneno ya Hassan ni kuzuia hilo moja kwa moja; kwasababu hakuna anayeweza kuuondoa uchawi isipokuwa mwenye maarifa ya uchawi, na hii inachukuliwa katika kuondoa uchawi kwa uchawi mfano wake, ambayo ni katika kazi za shetani, na aliweka wazi bin Qayyim kwa kusema: Nikuwa, kumtibu aliyerogwa kwa madawa ya halali na kusoma qur'ani ni jambo linalofaa, na kumtibu aliyerogwa kwa uchawi ni haramu.

Marejeo

1-فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، مطبعة السنة المحمدية، القاهرة، مصر، الطبعة: السابعة، 1377هـ - 1957م. 2-القول المفيد على كتاب التوحيد، دار ابن الجوزي، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الثانية, محرم، 1424هـ. 3-الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ - 2001م. 4-الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م. 5-التمهيد لشرح كتاب التوحيد، دار التوحيد، تاريخ النشر: 1424هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa

عن عمران بن حصين رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «‌لَيْسَ ‌مِنَّا ‌مَنْ ‌تَطَيَّرَ أَوْ تُطُيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ، وَمَنْ عَقَدَ عُقْدَةً، وَمَنْ أَتَى كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ».
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
Imepokelewa na AlbazzarDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Katoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mwayo: La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo. La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake. La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kumtegemea Allah na kuamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, na kuharamishwa kwa imani za mikosi na nuksi na uchawi na ukuhani, au kuwauliza wenye mambo hayo.
  2. Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
  3. Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.
Marejeo

مسند البزار = البحر الزخار (9/ 52) (3578). شرح السنة للبغوي (12/ 182). مجموع الفتاوى (35/ 173). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 543). التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص315). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص242). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص217).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «من اقتبَسَ علْمًا مِنَ النُّجُومِ اقْتبَسَ شُعبَة مِن السِّحرِ، زادَ ما زادَ».
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.

Mafunzo
  1. Uharamu wa unajimu ambao ni kueleza mambo yajayo kwa kutegemea hali za nyota; hili kwa sababu ni katika kudai elimu ya ghaibu.
  2. Kwa hakika unajimu ulioharamishwa ni katika aina za uchwi zinazopingana na tahuhidi, tofauti na kuzitazama nyota kwa ajili ya kujua uelekeo au kibla au kuingia kwa msimu na miezi haya ni halali.
  3. Kila anavozidisha katika kujifunza ndivyo anavyozidi kujifunza sehemu ya uchawi.
  4. Nyota zinafaida tatu amezitaja Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake: Ni pambo la mbingu, na ni alama hutumika kuongozea, na kipigo kwa mashetani
Marejeo

سنن أبي داود (6/ 50) (3905). سنن ابن ماجه (4/ 670) (3726). مسند أحمد (3/ 454) (2000). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص230). الملخص في شرح كتاب التوحيد، للفوزان (ص206).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

"Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,

Mafunzo
  1. Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
  2. Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
  3. Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
  4. Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
  5. Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 169) (846)، صحيح مسلم (1/ 83) (71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 484)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 260).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala

عن جابرٍ رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكَ الصَّلَاةِ».
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafiri ni kuacha swala, swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu, na jambo lake ni kubwa katika Uislamu, atakayeiacha kwa kupinga uwajibu wake amekufuru kwa makubaliano ya waislamu, na akiiacha moja kwa moja kwa uzembe na uvivu pia ni kafiri, na yamenukuliwa makubaliano ya Masahaba juu ya hilo, na ikiwa anaiacha baadhi ya wakati na wakati mwingine anaswali, basi anajitia katika makemeo haya makubwa.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa swala na kuihifadhi, kwani ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na imani.
  2. Tahadhari kubwa kwa atakayeacha swala na akaitelekeza.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 88) (82)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 271)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 622).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri

عن بريدة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ الْعَهْدَ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلَاةُ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa jambo la swala, nakuwa ndio kitenganishi kati ya waumini na makafiri.
  2. Kudhihiri hukumu za Uislamu kwa muonekano wa hali ya mtu pasina ndani ya moyo wake.
Marejeo

سنن النسائي (1/ 231) (463)، سنن الترمذي (4/ 365) (2621)، سنن ابن ماجه (2/ 181) (1079)، مسند أحمد (38/ 20) (22937)، فيض القدير (4/ 395)، ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (6/ 192) (6/ 193).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com