Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «من اقتبَسَ علْمًا مِنَ النُّجُومِ اقْتبَسَ شُعبَة مِن السِّحرِ، زادَ ما زادَ».
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.
Mafunzo
Uharamu wa unajimu ambao ni kueleza mambo yajayo kwa kutegemea hali za nyota; hili kwa sababu ni katika kudai elimu ya ghaibu.
Kwa hakika unajimu ulioharamishwa ni katika aina za uchwi zinazopingana na tahuhidi, tofauti na kuzitazama nyota kwa ajili ya kujua uelekeo au kibla au kuingia kwa msimu na miezi haya ni halali.
Kila anavozidisha katika kujifunza ndivyo anavyozidi kujifunza sehemu ya uchawi.
Nyota zinafaida tatu amezitaja Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake: Ni pambo la mbingu, na ni alama hutumika kuongozea, na kipigo kwa mashetani
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 50) (3905).
سنن ابن ماجه (4/ 670) (3726).
مسند أحمد (3/ 454) (2000).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص230).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، للفوزان (ص206).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com