Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala

عن جابرٍ رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكَ الصَّلَاةِ».
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafiri ni kuacha swala, swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu, na jambo lake ni kubwa katika Uislamu, atakayeiacha kwa kupinga uwajibu wake amekufuru kwa makubaliano ya waislamu, na akiiacha moja kwa moja kwa uzembe na uvivu pia ni kafiri, na yamenukuliwa makubaliano ya Masahaba juu ya hilo, na ikiwa anaiacha baadhi ya wakati na wakati mwingine anaswali, basi anajitia katika makemeo haya makubwa.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa swala na kuihifadhi, kwani ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na imani.
  2. Tahadhari kubwa kwa atakayeacha swala na akaitelekeza.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 88) (82)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 271)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 622).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Vitenguzi vya uislamu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com