Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Uzushi.

Hadithi 5

Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الْأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلَالَةٍ كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الْإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئًا».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.

Mafunzo
  1. Fadhila za kuwaita watu katika uongofu, uwe mdogo au mkubwa, na kuwa mwenye kuwaita watu katika uongofu ana malipo mfano wa malipo ya mfanyaji, na hilo ni katika fadhila kubwa za Allah na ukarimu wake uliokamilika.
  2. Hatari ya kuhamasisha upotofu, uwe kidogo au mwingi, nakuwa mwenye kuhimiza katika upotofu ana madhambi mfano wa mfanyaji.
  3. Malipo huendana na matendo, atakayelingania katika kheri atapata malipo mfano wa mfanyaji wake, na atakayelingania katika shari atapata mfano wa madhambi ya mfanyaji wake.
  4. Ni juu ya muislamu atahadhari kwa wale wenye kumuiga kwa kudhihirisha kwake maasi na watu wakimuona, kwani anapata dhambi kupitia atakayemuiga hata kama hajamhamasisha juu ya hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2060) (2674). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 262). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص141). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 360). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 554). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 199).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayezua katika dini yetu hii, yale yasiyokuwemo, basi yatarejeshwa

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ فِيهِ فَهُوَ رَدٌّ» متفق عليه. ولمسلم: «مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayezua katika dini yetu hii, yale yasiyokuwemo, basi yatarejeshwa" Kaipokea Bukhari na Muslim. Na kutoka kwa Muslim: "Atakayefanya amali yoyote isiyokuwa na amri yetu, basi itarejeshwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalili yoyote kutoka katika Qur'ani na Sunna, basi jambo hilo litarejeshwa kwa mfanyaji wake na halitokubaliwa mbele ya Allah.

Mafunzo
  1. Ibada zote zimejengeka juu ya yale yalikuja katika Qur'ani na Sunna, hatutakiwi kumuabudu Allah Mtukufu isipokuwa kwa sheria aliyoiweka na si kwa uzushi na mambo ya kutungwa.
  2. Dini haiendi kwa rai na kutazama lipi zuri, bali inakwenda kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  3. Hadithi hii ni ushahidi wa kukamilika dini.
  4. Uzushi ni kila kilichozushwa katika dini na hakikuwepo katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Masahaba zake katika itikadi (Aqida) au kauli au amali yoyote.
  5. Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, nayo ni sawa na mzani kwa matendo, kama ambavyo kila amali ambayo haikukusudiwa kupata radhi za Allah Mtukufu, mfanyaji wake hana thawabu ndani yake, hivyo hivyo kila amali ambayo haitakuwa samabamba na yale aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi hiyo itarejeshwa kwa mfanyaji wake.
  6. Uzushi uliokatazwa ni ule unaokuwa katika mambo ya dini na si ya kidunia.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 184) (2697). صحيح مسلم (3/ 1343) (1718). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص16). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص96). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص38).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakayezua (kitu) katika jambo letu hili (dini) ambalo si miongoni mwake, basi hilo litakataliwa

عَنْ أُمِّ المُؤْمِنِينَ أُمِّ عَبْدِ اللَّهِ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: قَالَ: رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: «مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ». وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: «مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ».
Kutoka kwa mama wa waumini mama Abdillah Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Yeyote atakayezua (kitu) katika jambo letu hili (dini) ambalo si miongoni mwake, basi hilo litakataliwa." Na katika riwaya nyingine ya Imamu Muslim: "Atakayefanya amali yoyote isiyokuwa na amri yetu basi itakataliwa".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalili yoyote kutoka katika Qur'ani na Sunna, basi jambo hilo litarejeshwa kwa mfanyaji wake na halitokubaliwa mbele ya Allah.

Mafunzo
  1. Ibada zote zimejengeka juu ya yale yalikuja katika Qur'ani na Sunna, hatutakiwi kumuabudu Allah Mtukufu isipokuwa kwa sheria aliyoiweka na si kwa uzushi na mambo ya kutungwa.
  2. Dini haiendi kwa rai na kutazama lipi zuri, bali inakwenda kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  3. Hadithi hii ni ushahidi wa kukamilika dini.
  4. Uzushi ni kila kilichozushwa katika dini na hakikuwepo katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Masahaba zake katika itikadi (Aqida) au kauli au amali yoyote.
  5. Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, nayo ni sawa na mzani kwa matendo, kama ambavyo kila amali ambayo haikukusudiwa kupata radhi za Allah Mtukufu, mfanyaji wake hana thawabu ndani yake, hivyo hivyo kila amali ambayo haitakuwa samabamba na yale aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi hiyo itarejeshwa kwa mfanyaji wake.
  6. Hadithi hii ndiyo kanuni katika kukataa uzushi na mambo mageni na maovu yanayotokea.
  7. Uzushi uliokatazwa ni ule unaokuwa katika mambo ya dini na si ya kidunia.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 184) (2697). صحيح مسلم (3/ 1343) (1718). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص16). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص96). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص38).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com