Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.
- Fadhila za kuwaita watu katika uongofu, uwe mdogo au mkubwa, na kuwa mwenye kuwaita watu katika uongofu ana malipo mfano wa malipo ya mfanyaji, na hilo ni katika fadhila kubwa za Allah na ukarimu wake uliokamilika.
- Hatari ya kuhamasisha upotofu, uwe kidogo au mwingi, nakuwa mwenye kuhimiza katika upotofu ana madhambi mfano wa mfanyaji.
- Malipo huendana na matendo, atakayelingania katika kheri atapata malipo mfano wa mfanyaji wake, na atakayelingania katika shari atapata mfano wa madhambi ya mfanyaji wake.
- Ni juu ya muislamu atahadhari kwa wale wenye kumuiga kwa kudhihirisha kwake maasi na watu wakimuona, kwani anapata dhambi kupitia atakayemuiga hata kama hajamhamasisha juu ya hilo.
صحيح مسلم (4/ 2060) (2674). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 262). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص141). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 360). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 554). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 199).