عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: إِذَا حَدَّثْتُكُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَأَنْ أَخِرَّ مِنَ السَّمَاءِ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَكْذِبَ عَلَيْهِ، وَإِذَا حَدَّثْتُكُمْ فِيمَا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ فَإِنَّ الحَرْبَ خَدْعَةٌ، سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «يَأْتِي فِي آخِرِ الزَّمَانِ قَوْمٌ حُدَثَاءُ الأَسْنَانِ سُفَهَاءُ الأَحْلاَمِ، يَقُولُونَ مِنْ خَيْرِ قَوْلِ البَرِيَّةِ، يَمْرُقُونَ مِنَ الإِسْلاَمِ كَمَا يَمْرُقُ السَّهْمُ مِنَ الرَّمِيَّةِ، لاَ يُجَاوِزُ إِيمَانُهُمْ حَنَاجِرَهُمْ، فَأَيْنَمَا لَقِيتُمُوهُمْ فَاقْتُلُوهُمْ، فَإِنَّ قَتْلَهُمْ أَجْرٌ لِمَنْ قَتَلَهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ».
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake: Nikikuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi kuporomoka kutoka mbinguni ni bora zaidi kwangu kuliko kumsemea uongo, na nikikuhadithieni katika yale yaliko baina yangu na nyinyi basi tambueni kuwa vita ni ulaghai (uongo), nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, imani yao haitovuka koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo siku ya Kiyama kwa atakayewaua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba, mtakaponisikia ninakuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi hakika mimi sifichi wala sibuni, wala sifuniki haki, bali ninaweka wazi, na kuanguka kwangu kutoka juu mbinguni ni rahisi na ni bora sana kwangu kuliko kusimulia jambo la uongo nikasema kuwa limetoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na nikisimulia mambo yalio kati yangu mimi na watu wengine, basi vita ni udanganyifu, hapo ninaweza kusema kwa mafumbo au kubuni au kuficha, kwani nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Watatokea katika zama za mwisho vijana wenye umri mdogo, wasiojitambua (madhaifu wa akili) watakuwa wakisema maneno kutoka ndani ya Qur'ani na wakiisoma kwa wingi, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu na wakivuka mipaka yake, kama mshale utokavyo katika upinde, Imani yao haivuki koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo kwa atakayewauwa, siku ya Kiyama.
Mafunzo
- Hapa kumebainishwa sifa miongoni mwa sifa za Makhawariji (wanao asi tawala zao).
- Katika hadithi hii kuna alama miongoni mwa alama za unabii, kiasi ambacho ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo yatakayotokea baada yake ndani ya Umma wake, na imetokea kama alivyoeleza.
- Kufaa kuleta mafumbo na hadaa katika vita, na udanganyifu katika vita unakuwa kwa mafumbo, na unakuwa kwa kuficha, na mfano wake, pasina kuvunja ahadi na amani, kwa kuja kwa katazo katika hilo.
- Amesema Nawawi katika neno "Wanazungumza kwa maneno bora kuliko yote" Maana yake: Inavyoonekana ni kama kauli yao: Hakuna hukumu isipokuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu, na mfano wa hilo katika madai yao ya kuwaleta watu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Haivuki imani yao koromeo zao": Makusudio yake nikuwa imani haijakita ndani ya nyoyo zao; kwa sababu kinachosimama katika koo bila kuvuka hakifiki ndani ya moyo.
- Amesema Kadhi: Wamekubaliana wanachuoni wote kuwa Makhawariji na mfano wao ni katika watu wazushi na waovu, wakati wowote watakapotoka kwa kiongozi na wakaenda kinyume na mtazamo wa watu wengi, na wakapasua umoja, basi ni wajibu kupigana nao baada ya kuwaonya, na kuwapa udhuru.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 200) (3611).
صحيح مسلم (2/ 746) (1066).
النهاية في غريب الحديث والأثر (259)(866).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (20/ 264) (20/ 258).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (6/ 58).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعًا لِمَا جِئْتُ بِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammadi Abdallahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".
Imepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimuliziDarajaAmesema Nawawi: Hadithi hii ni sahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanadam hawezi kuwa muumini mwenye imani kamili ya wajibu mpaka mapenzi yake yafuate yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa amri na makatazo na mengineyo, ayapende aliyoamrishwa, na ayachukie aliyokatazwa.
Mafunzo
- Hadithi hii ni kanuni ya kujisalimisha katika sheria na kutii.
- Tahadhari kwa mwanadamu kuwa yeyote mwenye kuipa kipaumbele akili au mazoea na akaitanguliza kuliko yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi huyu imani kwake imekanushwa.
- Ulazima wa kuifanya sheria kuwa ndio muamuzi katika kila kitu, kwa kauli yake: "Yale niliyokuja nayo".
- Nikuwa imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kumuasi.
Marejeo
الحجة على تارك المحجة لأبي الفتح نصر بن إبراهيم المقدسي، برقم (25).
فتح الباري لابن حجر (13/289).
جامع العلوم والحكم (3/1146).
شرح النووي على مسلم (1/77).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com