عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ: الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى الْمَيِّتِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni:
La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao.
La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.
Mafunzo
- Himizo la unyenyekevu na kutokujikweza kwa watu
- Ulazima wa kusubiri juu ya msiba na kutolalamika.
- Matendo haya ni katika ukafiri mdogo, na si kwamba mwenye kufanya sehemu katika sehemu za ukafiri anakuwa kafiri ukafiri unaomtoa mtu katika mila ya Uislamu mpaka umthibitikie ukafiri mkubwa.
- Uislamu umekataza mambo yote yanayopelekea kutengana baina ya waislamu kama kutukana nasaba na mengineyo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 82) (67).
كتاب التوحيد، للإمام محمد بن عبد الوهاب (ص96).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص279).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص315).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لاَ يَرْمِي رَجُلٌ رَجُلًا بِالفُسُوقِ، وَلاَ يَرْمِيهِ بِالكُفْرِ، إِلَّا ارْتَدَّتْ عَلَيْهِ، إِنْ لَمْ يَكُنْ صَاحِبُهُ كَذَلِكَ».
Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyosema, basi yeye ndiye atakayestahiki sifa iliyotajwa, na kauli yake itarudi kwake, na ama akiwa kama alivyosema basi hakuna kitakachorejea kwake; kwa sababu atakuwa mkweli katika hayo aliyoyasema.
Mafunzo
- Uharamu wa kuwatuhumu watu kwa ukafiri au uovu, pasina sababu ya kisheria.
- Ulazima kupata uhakika katika utoaji wa hukumu kwa watu.
- Amesema bin Daqiq Al-Iddi: Na hii ni tahadhari kubwa kwa atakayemkufurisha yeyote katika waislamu haliyakuwa hayuko hivyo, na huku ni kujitia mtegoni kukubwa.
- Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Lakini haipelekei kutokuwa kwake muovu au kafiri kutokupata dhambi katika sura ya kauli yake: Wewe ni muovu, bali katika sura hii kuna mchanganuo: Ikiwa atakusudia kumnasihi au kumnasihi mtu mwingine kwa kubainisha hali yake hapa itafaa, na ikiwa atakusudia kumuaibisha na kumtangaza kwa hilo na kumuudhi haitafaa; kwa sababu ameamrishwa na sheria kumsitiri na kumueleimisha na kumpa mawaidha kwa njia nzuri, kwa namna yoyote itakayowezekana kwake kuitumia kwa upole basi haifai kwake kutumia ukali; kwa sababu inaweza kuwa sababu ya kumhadaa na kumfanya aendelee na hilo, kama ilivyo tabia ya baadhi ya watu pale upole usipotumika, na hasa hasa atapokuwa muamrishaji yuko chini ya muamriwa katika cheo.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 15) (6045).
صحيح مسلم (1/ 79) (61).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1073).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (18/ 446).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 82).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 220).
التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (9/ 275).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، ابْنُ جُدْعَانَ كَانَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ يَصِلُ الرَّحِمَ، وَيُطْعِمُ الْمِسْكِينَ، فَهَلْ ذَاكَ نَافِعُهُ؟ قَالَ: «لَا يَنْفَعُهُ، إِنَّهُ لَمْ يَقُلْ يَوْمًا: رَبِّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu Abdullahi Bin Jad'aan, na alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kikuraishi kabla ya Uislamu, Na miongoni mwa vitendo vyake vizuri ni kuwa yeye: huunganisha ndugu zake na huwafanyia wema, na hulisha chakula masikini, na mambo mengine mengi ambayo Uislamu umeyahimiza kuyafanya, nakuwa matendo haya hayatomfaa katika Akhera yake; Na hilo ni kwa sababu ya kumkufuru Mola wake, na kuwa yeye hajawahi hata siku moja kusema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi makosa yangu siku ya Kiyama.
Mafunzo
- Kuweka wazi utukufu na ubora wa imani, na kuwa imani ni sharti la kukubaliwa matendo yote.
- Kuweka wazi ubaya wa ukafiri, na kuwa ukafiri huporomosha matendo mema.
- Makafiri hayatawafaa matendo yao huko Akhera kwa sababu ya kutokumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.
- Matendo ya mwanadamu akiwa bado yupo kwenye ukafiri huandikiwa atakapo silimu na atalipwa kwa matendo hayo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 196) (214)، شرح النووي على مسلم (3/87)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 459)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (4/ 170)، التنوير شرح الجامع الصغير (2/364)، فتح المنعم (2/54)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (3/ 455).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,
Mafunzo
- Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
- Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
- Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
- Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
- Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 169) (846)، صحيح مسلم (1/ 83) (71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 484)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 260).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن جابرٍ رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكَ الصَّلَاةِ».
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafiri ni kuacha swala, swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu, na jambo lake ni kubwa katika Uislamu, atakayeiacha kwa kupinga uwajibu wake amekufuru kwa makubaliano ya waislamu, na akiiacha moja kwa moja kwa uzembe na uvivu pia ni kafiri, na yamenukuliwa makubaliano ya Masahaba juu ya hilo, na ikiwa anaiacha baadhi ya wakati na wakati mwingine anaswali, basi anajitia katika makemeo haya makubwa.
Mafunzo
- Umuhimu wa swala na kuihifadhi, kwani ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na imani.
- Tahadhari kubwa kwa atakayeacha swala na akaitelekeza.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 88) (82)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 271)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 622).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن بريدة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ الْعَهْدَ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلَاةُ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.
Mafunzo
- Ukubwa wa jambo la swala, nakuwa ndio kitenganishi kati ya waumini na makafiri.
- Kudhihiri hukumu za Uislamu kwa muonekano wa hali ya mtu pasina ndani ya moyo wake.
Marejeo
سنن النسائي (1/ 231) (463)، سنن الترمذي (4/ 365) (2621)، سنن ابن ماجه (2/ 181) (1079)، مسند أحمد (38/ 20) (22937)، فيض القدير (4/ 395)، ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (6/ 192) (6/ 193).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com