Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ: الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى الْمَيِّتِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni: La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao. La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.

Mafunzo
  1. Himizo la unyenyekevu na kutokujikweza kwa watu
  2. Ulazima wa kusubiri juu ya msiba na kutolalamika.
  3. Matendo haya ni katika ukafiri mdogo, na si kwamba mwenye kufanya sehemu katika sehemu za ukafiri anakuwa kafiri ukafiri unaomtoa mtu katika mila ya Uislamu mpaka umthibitikie ukafiri mkubwa.
  4. Uislamu umekataza mambo yote yanayopelekea kutengana baina ya waislamu kama kutukana nasaba na mengineyo.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 82) (67). كتاب التوحيد، للإمام محمد بن عبد الوهاب (ص96). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص279). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص315).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kufuru

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com