عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «بَادِرُوا بِالْأَعْمَالِ فِتَنًا كَقِطَعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرَّجُلُ مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، أَوْ يُمْسِي مُؤْمِنًا وَيُصْبِحُ كَافِرًا، يَبِيعُ دِينَهُ بِعَرَضٍ مِنَ الدُّنْيَا».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamtaka Muumini kufanya hima na kufanya mambo mengi ya kheri kabla hayajashindikana, na akashughulishwa na kuja kwa fitna na mambo yenye kutatiza yanayoweza kuzuia kufanya matendo mema, na kuyaziba, na hali ni kwamba, ni giza kama kipande cha usiku ambao ndani yake haki imechanganyika na batili, na kukawawia vigumu watu kutofautisha baina yake, na kwa sababu ya ukali wake (Fitina hiyo), mtu huchanganyikiwa kiasi cha kuamka muumini, na kufika jioni ni kafiri, kushinda Muumini na kufika asubuhi kawa kafiri, anaiacha dini yake kwa starehe za muda mfupi za dunia.
Mafunzo
- Ni lazima kushikamana na dini, na kwenda mbio katika matendo mema kabla ya vikwazo kuzuia hilo.
- Hii ni ishara ya mfuatano wa majaribu yenye kupoteza katika zama za mwisho, na kwamba wakati wowote fitina moja inapotoweka, fitina ingine linafuata.
- Ikiwa dini ya mtu ni dhaifu na akaiacha kwa kubadilishana na mambo ya kidunia, kama vile pesa au vitu vingine, hii ni sababu ya kupotoka kwake, kuacha dini, na kuingia kwake kwenye vishawishi na fitina.
- Kuna ushahidi katika Hadithi kwamba matendo mema ni njia ya kuokoka na fitina.
- Kuna aina mbili za fitina: Fitina ya shubuha (Mambo yenye utata), na tiba yake ni elimu, na fitina ya matamanio, na tiba yake ni imani na subira.
- Hadithi inaashiria kuwa mwenye matendo kidogo, fitina kwake ni nyepesi zaidi, na mwenye matendo mengi anatakiwa asihadaike na alichonacho, bali aongeze zaidi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 110) (118).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 169).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 16).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 122).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه: عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ فِي الْأَنْصَارِ: «لَا يُحِبُّهُمْ إِلَّا مُؤْمِنٌ، وَلَا يُبْغِضُهُمْ إِلَّا مُنَافِقٌ، مَنْ أَحَبَّهُمْ أَحَبَّهُ اللهُ وَمَنْ أَبْغَضَهُمْ أَبْغَضَهُ اللهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Allah ziwe juu yake: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa, kuwapenda Manswari katika watu wa Madina, ni alama ya ukamilifu wa imani; na hii ni kwa sababu ya kuwahi kwao kuutetea Uislamu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuleta amani pia, na kwenda kwao mbio kuwapa hifadhi waislamu, na kutoa kwao mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, nakuwa kuwachukia ni alama ya unafiki. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayewapenda Manswari Mwenyezi Mungu humpenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu humchukia.
Mafunzo
- Kuna nafasi kubwa ya Manswari, kuwapenda kwao ni alama ya imani na ni kujiweka mbali na unafiki.
- Kuwapenda vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwatetea ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumpenda mja.
- Fadhila na ubora wa wale waliotangulia katika Uislamu.
Marejeo
صحيح البخاري (5/ 32) (3783).
صحيح مسلم (1/ 85) (75).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 447).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص257).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 258).
شرح النووي على مسلم (2/ 63).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 350).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن جابر رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَرَأَيْتَ إِذَا صَلَّيْتُ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ، وَصُمْتُ رَمَضَانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلَالَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ؟ قَالَ: «نَعَمْ»، قَالَ: وَاللهِ لَا أَزِيدُ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا.
Hadithi imepokelewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo", Akasema mtu yule: "Namuapia Mwenyezi Mungu sizidishi zaidi ya matendo hayo kitu chochote".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.
Mafunzo
- Muislamu kupupia juu ya kufanya mambo yaliyo faradhishwa na kuacha yaliyoharamishwa, na yawe malengo yake ni kuingia peponi.
- Umuhimu wa kufanya yaliyo halali na kuamini uhalali wake, na kuharamisha yaliyo haramu na kuamini uharamu wake.
- Kufanya yaliyo wajibu na kuacha yaliyo haramu ni sababu za kuingia Peponi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 44) (15).
جامع العلوم والحكم (1/513). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 215).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 77).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي مالكٍ الأشعريِّ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَآنِ -أَوْ تَمْلَأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا».
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.
Mafunzo
- Twahara zipo aina mbili: Twahara ya nje nayo ni udhu na kuoga, na twahara ya ndani inakuwa kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuwa na imani na matendo mazuri.
- umuhimu wa kuzihifadhi swala tano, kwakuwa swala tano ni mwangaza kwa mja hapa Duniani na siku ya Kiyama.
- Kutoa sadaka ni dalili ya imani ya kweli.
- Umuhimu wa kuifanyia kazi Qur'ani na kuisadikisha ili iwe ni hoja kwako au dhidi yako.
- Ikiwa nafsi hutoishughulisha na utiifu itakushughulisha na maasi.
- Kila mwanadamu lazima afanye matendo, hivyo ima aikomboe nafsi yake kwa kutii, au aiangamize kwa kufanya maasi.
- Na subira inahitaji uvumilivu na kutarajia thawabu, na ndani yake kuna uzito.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 203) (223)، شرح الأربعين لابن دقيق العيد (ص 84)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 231)، الرياض الزكية شرح الأربعين النووية للخضير (ص 293)، فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 79)
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,
Mafunzo
- Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
- Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
- Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
- Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
- Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 169) (846)، صحيح مسلم (1/ 83) (71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 484)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 260).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَتْ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي عَلَى الحَوْضِ حَتَّى أَنْظُرَ مَنْ يَرِدُ عَلَيَّ مِنْكُمْ، وَسَيُؤْخَذُ نَاسٌ دُونِي، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ مِنِّي وَمِنْ أُمَّتِي، فَيُقَالُ: هَلْ شَعَرْتَ مَا عَمِلُوا بَعْدَكَ، وَاللَّهِ مَا بَرِحُوا يَرْجِعُونَ عَلَى أَعْقَابِهِمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Asmaa Bint Abii Bakari-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa siku ya Kiyama yeye atakuwa kwenye Birika lake ili amuone kila mwenye kuja kwenye Birika katika watu wa umma wake. Na watachukuliwa watu wakiwa karibu na Mtume -Amani iwe juu yake- basi atasema: Ewe Mola wangu hao ni wangu na nikatika umma wangu, Basi kutasemwa: Je unajua walichofanya baada ya wewe kuachana nao? Namuapia Mwenyezi Mungu hawakuwacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao, hivyo basi hao siyo watu wako wala si katika umma wako.
Mafunzo
- Huruma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kwa umma wake na kuwatilia umuhimu.
- Hatari ya kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake.
- Himizo la kushikamana na sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 121) (6593)، صحيح مسلم (4/ 1793) (2292)، عمدة القاري (23/144)، البحر المحيط الثجاج (37/322).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com