عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَتْ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي عَلَى الحَوْضِ حَتَّى أَنْظُرَ مَنْ يَرِدُ عَلَيَّ مِنْكُمْ، وَسَيُؤْخَذُ نَاسٌ دُونِي، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ مِنِّي وَمِنْ أُمَّتِي، فَيُقَالُ: هَلْ شَعَرْتَ مَا عَمِلُوا بَعْدَكَ، وَاللَّهِ مَا بَرِحُوا يَرْجِعُونَ عَلَى أَعْقَابِهِمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Asmaa Bint Abii Bakari-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa siku ya Kiyama yeye atakuwa kwenye Birika lake ili amuone kila mwenye kuja kwenye Birika katika watu wa umma wake. Na watachukuliwa watu wakiwa karibu na Mtume -Amani iwe juu yake- basi atasema: Ewe Mola wangu hao ni wangu na nikatika umma wangu, Basi kutasemwa: Je unajua walichofanya baada ya wewe kuachana nao? Namuapia Mwenyezi Mungu hawakuwacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao, hivyo basi hao siyo watu wako wala si katika umma wako.
Mafunzo
- Huruma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kwa umma wake na kuwatilia umuhimu.
- Hatari ya kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake.
- Himizo la kushikamana na sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 121) (6593)، صحيح مسلم (4/ 1793) (2292)، عمدة القاري (23/144)، البحر المحيط الثجاج (37/322).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com