Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Unafiki.

Hadithi 4

Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «‌إِنَّ ‌أَثْقَلَ صَلَاةٍ عَلَى الْمُنَافِقِينَ صَلَاةُ الْعِشَاءِ وَصَلَاةُ الْفَجْرِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا، وَلَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَتُقَامَ، ثُمَّ آمُرَ رَجُلًا فَيُصَلِّيَ بِالنَّاسِ، ثُمَّ أَنْطَلِقَ مَعِي بِرِجَالٍ مَعَهُمْ حُزَمٌ مِنْ حَطَبٍ إِلَى قَوْمٍ لَا يَشْهَدُونَ الصَّلَاةَ، فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ بِالنَّارِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wanafiki na uvivu wao wa kuhudhuria swala, hasa hasa swala mbili, Ishaa na Alfajiri, nakuwa laiti wangelijua kiwango cha malipo na thawabu katika kuzihudhuria swala hizo pamoja na jamaa ya waislamu, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa mfano wa kutambaa kwa mtoto kwa mikono na magoti. Bila shaka aliazimia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aamrishe swala ikimiweisimamishwe), na amuweke mtu awasalishe watu badala yake, kisha aondoke akiwa pamoja na watu watakaombebea mizigo ya kuni kwenda kwa watu wasiohudhuria swala ya pamoja (Jamaa) ili awachome wakiwa ndani ya majumba yao; kwa sababu ya ubaya wa waliyoyafanya katika madhambi, -lakini hakufanya hivyo- kwa sababu ndani ya majumba yao kuna wanawake na watoto wasio na hatia, na wengineo miongoni mwa wenye udhuru, wasiokuwa na dhambi.

Mafunzo
  1. Hatari ya kuchelewa swala ya pamoja msikitini.
  2. Wanafiki hawakukusudia katika ibada zao isipokuwa kujionyesha na kutaka kusikika, hawaji katika swala ila katika wakati ambao watu wanawaona.
  3. Malipo makubwa katika swala mbili, Ishaa na Alfajiri kwa jamaa, nakuwa swala hizo zinastahiki zaidi kuziendea hata kwa kutambaa.
  4. Kuhifadhi swala mbili, Ishaa na Alfajiri ni sababu ya kusalimika na unafiki, na kuto kuzihudhuria ni katika sifa za wanafiki.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 451) (651). صحيح البخاري (1/ 132) (657). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 88). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص107). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 136).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «مَثَلُ الْمُنَافِقِ، كَمَثَلِ الشَّاةِ الْعَائِرَةِ بَيْنَ الْغَنَمَيْنِ تَعِيرُ إِلَى هَذِهِ مَرَّةً وَإِلَى هَذِهِ مَرَّةً».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hali za wanafiki, na kuwa mnafiki ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga na asiyejua afuate kundi gani la Mbuzi, wakati mwingine huenda kundi hili na wakati mwingine huenda na kundi lingine, Wanafiki hutangatanga baina ya imani na ukafiri, hivyo hawapo na waumini kwa wazi wazi wala kwa kujificha, wala hawapo na makafiri kwa wazi wala kwa kujificha, bali kwa muonekano wa nje wanaonekana wapo na waumini, na kwa ndani (kwa siri) wapo kwenye shaka na kutanga tanga, wakati mwingine, na wakati mwingine wanaelemea kwa hawa na wakati mwingine kwenye kundi hili.

Mafunzo
  1. Miongoni mwa miongozo ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kupiga mfano ili kufahamu haraka.
  2. Kuweka wazi hali za wanafiki za kutangatanga kuwa na mashaka na kutokuwa na utulivu.
  3. Kuchukua tahadhari kutokana na hali za wanafiki na kuhimizwa kuwa na imani nje na ndani.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2146) (2784)، إكمال المعلم بفوائد مسلم (8/ 313)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (16/ 69).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما قال: قال رَسولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا خَالِصًا، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَلَّةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَلَّةٌ مِنْ نِفَاقٍ حَتَّى يَدَعَهَا: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Tabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa baadhi ya alama za mnafiki na tahadhari ya kutoangukia katika unafiki.
  2. Makusudio ya hadithi: Ni kuwa sifa hizi ni sifa za unafiki, na mwenye sifa hizi anafanana na wanafiki kwa sifa hizi, na amejipamba kwa tabia zao, haina maana kuwa ni mnafiki anayedhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa hii inachukuliwa kwa mtu ambaye zitakuwa nyingi kwake sifa hizi na akazipuuzia, na akaziona ndogo; basi atakayekuwa hivyo mara nyingi huwa kaharibika katika itikadi yake.
  3. Amesema Imam Ghazal: Msingi wa dini zote umekusanywa na mambo matatu: Kauli, kitendo, na nia, akatanabahisha kuwa kuharibika kwa maneno ni kwa uongo, na kuharibika kwa vitendo kunakuwa kwa hiyana, na kuharika kwa nia ni kwa kwenda kinyume; kwa sababu kwenda kinyume na ahadi hakumchafui mtu isipokuwa maazimio yake yatakapoambatanishwa na ahadi, ama atakapokusudia kisha kikamtokea kizuizi au akabadili mtazamo huyu hatokuwa na sura ya unafiki.
  4. Unafiki una aina mbili: Unafiki wa kiitikadi unamtoa mtu katika imani, nao ni kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na unafiki wa vitendo, nao ni kujifananisha na wanafiki katika tabia zao, na huu haumtoi mtu katika imani, isipokuwa ni dhambi katika madhambi makubwa.
  5. Amesema bin Hajari: Na wamekubaliana wanachuoni kuwa atakayesadikisha kwa moyo wake na ulimi wake na akafanya mambo haya hahukumiwi kwa ukafiri, wala si mnafiki atakayekaa motoni milele.
  6. Amesema Imam Nawawi: Na wamesema wanachuoni wengi kuwa: Makusudio yake ni wanafiki waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walizungumza kwa imani yao, na wakapinga, na wakaaminiwa kwa dini yao wao wakafanya hiyana, na wakaahidi katika swala la dini na kuinusuru, wakaenda kinyume, na wakavuka mipaka katika ugomvi wao.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 16) (34)، صحيح مسلم (1/ 78) (58)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 250)، بهجة قلوب الأبرار (ص 26)، البحر المحيط الثجاج (2/370).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما قال: قال رَسولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا، وَإِنْ كَانَتْ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ فِيهِ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا: مَنْ إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وإذَا خَاصَمَ فَجَرَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Tabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa baadhi ya alama za mnafiki na tahadhari ya kutoangukia katika unafiki.
  2. Makusudio ya hadithi: Ni kuwa sifa hizi ni sifa za unafiki, na mwenye sifa hizi anafanana na wanafiki kwa sifa hizi, na amejipamba kwa tabia zao, haina maana kuwa ni mnafiki anayedhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa hii inachukuliwa kwa mtu ambaye zitakuwa nyingi kwake sifa hizi na akazipuuzia, na akaziona ndogo; basi atakayekuwa hivyo mara nyingi huwa kaharibika katika itikadi yake.
  3. Amesema Imam Ghazal: Msingi wa dini zote umekusanywa na mambo matatu: Kauli, kitendo, na nia, akatanabahisha kuwa kuharibika kwa maneno ni kwa uongo, na kuharibika kwa vitendo kunakuwa kwa hiyana, na kuharika kwa nia ni kwa kwenda kinyume; kwa sababu kwenda kinyume na ahadi hakumchafui mtu isipokuwa maazimio yake yatakapoambatanishwa na ahadi, ama atakapokusudia kisha kikamtokea kizuizi au akabadili mtazamo huyu hatokuwa na sura ya unafiki.
  4. Unafiki una aina mbili: Unafiki wa kiitikadi unamtoa mtu katika imani, nao ni kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na unafiki wa vitendo, nao ni kujifananisha na wanafiki katika tabia zao, na huu haumtoi mtu katika imani, isipokuwa ni dhambi katika madhambi makubwa.
  5. Amesema bin Hajari: Na wamekubaliana wanachuoni kuwa atakayesadikisha kwa moyo wake na ulimi wake na akafanya mambo haya hahukumiwi kwa ukafiri, wala si mnafiki atakayekaa motoni milele.
  6. Amesema Imam Nawawi: Na wamesema wanachuoni wengi kuwa: Makusudio yake ni wanafiki waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walizungumza kwa imani yao, na wakapinga, na wakaaminiwa kwa dini yao wao wakafanya hiyana, na wakaahidi katika swala la dini na kuinusuru, wakaenda kinyume, na wakavuka mipaka katika ugomvi wao.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 16) (34). صحيح مسلم (1/ 78) (58). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 250). بهجة قلوب الأبرار (ص 26). البحر المحيط الثجاج (2/370).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com