عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا السِّلَاحَ فَلَيْسَ مِنَّا».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya hivyo pasina haki, atakuwa ametenda kosa kubwa na dhambi miongoni mwa madhambi makubwa, na atakuwa kastahiki kemeo hili kali.
Mafunzo
Tahadhari kubwa ya waislamu kuwapiga ndugu zao waislamu.
Katika maovu makubwa na ufisadi mkubwa katika ardhi ni kutangaza silaha dhidi ya waislamu, na kufanya ufisadi kwa mauaji.
Kemeo lililotajwa halihusiani na kupigana kwa haki, kama kuwapiga waliokengeuka na mafisadi na wengineo.
Uharamu wa kuwatisha waislamu kwa silaha au kinginecho hata kama ni kwa sura ya mzaha.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 49) (7071).
صحيح مسلم (1/ 98) (100).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص406).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص815).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 195).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص752).
Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyosema, basi yeye ndiye atakayestahiki sifa iliyotajwa, na kauli yake itarudi kwake, na ama akiwa kama alivyosema basi hakuna kitakachorejea kwake; kwa sababu atakuwa mkweli katika hayo aliyoyasema.
Mafunzo
Uharamu wa kuwatuhumu watu kwa ukafiri au uovu, pasina sababu ya kisheria.
Ulazima kupata uhakika katika utoaji wa hukumu kwa watu.
Amesema bin Daqiq Al-Iddi: Na hii ni tahadhari kubwa kwa atakayemkufurisha yeyote katika waislamu haliyakuwa hayuko hivyo, na huku ni kujitia mtegoni kukubwa.
Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Lakini haipelekei kutokuwa kwake muovu au kafiri kutokupata dhambi katika sura ya kauli yake: Wewe ni muovu, bali katika sura hii kuna mchanganuo: Ikiwa atakusudia kumnasihi au kumnasihi mtu mwingine kwa kubainisha hali yake hapa itafaa, na ikiwa atakusudia kumuaibisha na kumtangaza kwa hilo na kumuudhi haitafaa; kwa sababu ameamrishwa na sheria kumsitiri na kumueleimisha na kumpa mawaidha kwa njia nzuri, kwa namna yoyote itakayowezekana kwake kuitumia kwa upole basi haifai kwake kutumia ukali; kwa sababu inaweza kuwa sababu ya kumhadaa na kumfanya aendelee na hilo, kama ilivyo tabia ya baadhi ya watu pale upole usipotumika, na hasa hasa atapokuwa muamrishaji yuko chini ya muamriwa katika cheo.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 15) (6045).
صحيح مسلم (1/ 79) (61).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1073).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (18/ 446).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 82).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 220).
التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (9/ 275).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com