Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا السِّلَاحَ فَلَيْسَ مِنَّا».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya hivyo pasina haki, atakuwa ametenda kosa kubwa na dhambi miongoni mwa madhambi makubwa, na atakuwa kastahiki kemeo hili kali.

Mafunzo
  1. Tahadhari kubwa ya waislamu kuwapiga ndugu zao waislamu.
  2. Katika maovu makubwa na ufisadi mkubwa katika ardhi ni kutangaza silaha dhidi ya waislamu, na kufanya ufisadi kwa mauaji.
  3. Kemeo lililotajwa halihusiani na kupigana kwa haki, kama kuwapiga waliokengeuka na mafisadi na wengineo.
  4. Uharamu wa kuwatisha waislamu kwa silaha au kinginecho hata kama ni kwa sura ya mzaha.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 49) (7071). صحيح مسلم (1/ 98) (100). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص406). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص815). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 195). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص752).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Uovu

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com