kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi wakamuuliza: kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Lilikuja kundi la maswahaba kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na wakamuuliza kuhusiana na yanayowatokea katika nafsi zao miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanakuwa kwao ni mazito kuyasema kutokana na ubaya wake na kupenda kwao kujiepusha nayo Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: kwa hakika hiki ambacho mnakipata kwenye nafsi zenu ndiyo imani ya kweli na uhakika ambao unawapa msukumo ili kuzuia anayoyaweka shetani katika nyoyo na kuwazuieni kuyasema na kuyaona ni mazito kwenye nafsi zenu, na shetani kutoweza kuimiliki mioyo yenu, tofauti na yule ambaye ametawaliwa na shetani kwenye moyo wake akashindwa kupata chenye kumzuia kusema .
Mafunzo
Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, pale ambapo shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
Kutokubali na kusadikisha kinachotakwa na nafsi miongoni mwa wasiwasi, kwani wasiwasi hutokana na shetani.
Wasiwasi wa Shetani haumdhuru muumini, lakini anatakiwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na wasiwasi wake, na aache kuendekeza wasiwasi.
Haipasi kwa muislamu kunyamazia mambo yenye kumtatiza miongoni mwa mambo yanayo husu dini yake, na anapasa kuuliza kuhusu hilo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 119) (132)، معالم السنن (4/174)، المفهم للقرطبي (1/344)، شرح النووي على مسلم (2/154)، البحر المحيط الثجاج (3/622).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com