Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka

Hadithi 80

Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu

عن عبد الله بن عباس رضي الله عنهما قال: "ما السماوات السبع والأرضون السبع في كَفِّ الرحمن إلا كَخَرْدَلَةٍ في يد أحدكم".
Kutoka kwa Abdillah bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu".
Imepokelewa na Ibnu Jariri - Imepokelewa na Adh-dhahaby katika kitabu cha Uluwwi - Imepokelewa na Abdallah bin Al-Imam AhmadDarajaAlbany amenukuu usahihi wake kutoka kwa Ibn Taymiyyah na hakuifatilia
Maelezo

Anatueleza Abdillahi bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika nukuu hii kuwa kiwango cha asilimia ya mbingu saba na ardhi saba pamoja na ukubwa wake katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa Rehema-, ni kama kiwango cha punje ndogo ya ulezi katika kiganja cha mmoja wetu, na hii ni kufananisha kiwango kwa kiwango, na si kufananisha kiganja kwa kiganja; kwasababu Mwenyezi Mungu sifa zake hazifanani na kitu chochote kama ambavyo dhati yake haifanani na chochote.

Marejeo

1- فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، مطبعة السنة المحمدية، القاهرة، مصر، الطبعة: السابعة، 1377هـ - 1957م. 2- القول المفيد على كتاب التوحيد، دار ابن الجوزي، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الثانية, محرم، 1424ه. 3- الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ - 2001م. 4- الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م. 5- التمهيد لشرح كتاب التوحيد، دار التوحيد، تاريخ النشر: 1424هـ. 6- جامع البيان في تأويل القرآن، المؤلف: محمد بن جرير أبو جعفر الطبري، المحقق: أحمد محمد شاكر، الناشر: مؤسسة الرسالة، الطبعة: الأولى، 1420هـ - 2000م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo

عَنْ عُبَادَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ، وَالْجَنَّةُ حَقٌّ، وَالنَّارُ حَقٌّ، أَدْخَلَهُ اللهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنَ الْعَمَلِ».
Kutoka kwa Ubada bin -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetamka neno la tauhidi kwa kujua maana yake, kwa kuyafanyia kazi madhumuni yake, na akashuhudia utumwa wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- na ujumbe wake, na akakiri utumwa wa Issa na ujumbe wake, Na kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba kwa kauli yake "Kuwa" na akawa, na kuwa yeye ni roho miongoni mwa roho alizoziumba Mwenyezi Mungu, Na akamtenga mbali mama yake kwa yale waliyomnasibisha nayo Mayahudi, Nakuwa atakayeamini pepo kuwa ni kweli, na kuwa Moto ni kweli, akaitakidi uwepo wake, nakuwa hizo ni neema za Mwenyezi Mungu na adhabu yake, Na atakayekufa katika imani hiyo; basi mafikio yake ni Peponi hata kama alikuwa mzembe katika ibada, na anamadhambi.

Mafunzo
  1. Mwenyezi Mungu Mtukufu kamuumba Issa mwana wa Mariamu kwa neno (Kuwa) bila baba.
  2. Kinachowakusanya pamoja kati ya Issa (Yesu) na Muhammadi amani iwe juu yao wote ni kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, basi wao wote wawili ni Mitume hawasemi uongo, na ni waja wala hawaabudiwi.
  3. Ubora wa tauhidi na kufuta kwake madhambi, nakuwa mafikio ya mtu wa tauhidi ni Peponi, hata kama yakajitokeza kwake baadhi ya madhambi.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 165) (3435). صحيح مسلم (1/ 57) (28). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص25). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص36).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".
Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineoDarajaAmesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.

Mafunzo
  1. Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upole wake kwa waja wake kiasi ambacho amewaondolea madhambi pale yatakapojitokeza maasi katika hali hizi tatu.
  2. Fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya umma wake.
  3. Kuondolewa dhambi haimaanishi kuondolewa hukumu au dhamana, mfano atakayesahau udhu, na akaswali kwa kudhani kuwa yuko twahara, hana dhambi katika hilo, lakini atatakiwa kutia udhu na kurudia swala.
  4. Lazima katika kuondolewa dhambi kwa kulazimishwa kuwe na sharti, mfano kama akiwa mlazimishaji anauwezo wa kutimiza alichotishia.
Marejeo

الأربعون النووية (ص127) (ح39). سنن ابن ماجه (3/ 200) (2045). السنن الكبرى للبيهقي (7/ 584) (15094). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص89). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص382).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Umejengwa uislamu kwa mambo matano

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَر رضي الله عنهما قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: «بُنِيَ الْإِسْلَامُ عَلَى خَمْسٍ: شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَإِقَامِ الصَّلَاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، وَحَجِّ الْبَيْتِ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ».
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.

Mafunzo
  1. Nguzo mbili zinakwenda sambamba, haikubaliki moja mpaka iwe na nyingine; ndio maana akazifanya kuwa nguzo moja.
  2. Shahada mbili ndio msingi wa Dini, haikubaliki kauli wala amali ila kwa shahada hizo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 11) (8)، صحيح مسلم (1/ 45) (16)، و(1/ 88) (82)، فتح الباري لابن رجب (1/ 22)، جامع العلوم والحكم (1/147)، شرح الأربعين لابن العطّار (ص 62)، شرح الأربعين النووية لعبد الكريم الخضير (ص 87)، فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 29)، شرح الأربعين النووية لصالح آل الشيخ (ص 91 - 95)، التحفة الربانية لإسماعيل الأنصاري (ص 12).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا الْمُوجِبَتَانِ؟ فَقَالَ: «مَنْ مَاتَ لَا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ»
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.

Mafunzo
  1. Ubora wa Tauhidi na kuwa yeyote atakaye kufa hali yakuwa ni muumini wa kweli hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi.
  2. Hatari ya ushirikina, nakuwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni.
  3. Wafanya maasi wale wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 94) (93)، إكمال المعلم بفوائد مسلم (1/ 363)، شرح النووي على مسلم (2/96) المفهم للقرطبي (1/290)، تطريز رياض الصالحين (ص 281)، الكوكب الوهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج (3/63).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: جَاءَ نَاسٌ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَسَأَلُوهُ: إِنَّا نَجِدُ فِي أَنْفُسِنَا مَا يَتَعَاظَمُ أَحَدُنَا أَنْ يَتَكَلَّمَ بِهِ، قَالَ: «وَقَدْ وَجَدْتُمُوهُ؟» قَالُوا: نَعَمْ، قَالَ: «ذَاكَ صَرِيحُ الْإِيمَانِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi wakamuuliza: kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Lilikuja kundi la maswahaba kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na wakamuuliza kuhusiana na yanayowatokea katika nafsi zao miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanakuwa kwao ni mazito kuyasema kutokana na ubaya wake na kupenda kwao kujiepusha nayo Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: kwa hakika hiki ambacho mnakipata kwenye nafsi zenu ndiyo imani ya kweli na uhakika ambao unawapa msukumo ili kuzuia anayoyaweka shetani katika nyoyo na kuwazuieni kuyasema na kuyaona ni mazito kwenye nafsi zenu, na shetani kutoweza kuimiliki mioyo yenu, tofauti na yule ambaye ametawaliwa na shetani kwenye moyo wake akashindwa kupata chenye kumzuia kusema .

Mafunzo
  1. Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, pale ambapo shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
  2. Kutokubali na kusadikisha kinachotakwa na nafsi miongoni mwa wasiwasi, kwani wasiwasi hutokana na shetani.
  3. Wasiwasi wa Shetani haumdhuru muumini, lakini anatakiwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na wasiwasi wake, na aache kuendekeza wasiwasi.
  4. Haipasi kwa muislamu kunyamazia mambo yenye kumtatiza miongoni mwa mambo yanayo husu dini yake, na anapasa kuuliza kuhusu hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 119) (132)، معالم السنن (4/174)، المفهم للقرطبي (1/344)، شرح النووي على مسلم (2/154)، البحر المحيط الثجاج (3/622).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: جاءَ رجُلُ إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسولَ اللهِ، إن أحدنا يجدُ في نفسِهِ -يُعرِّضُ بالشَّيءِ- لأَن يكونَ حُمَمَةً أحَبُّ إليه من أن يتكلَّم بِهِ، فقال: «اللهُ أكبرُ، اللهُ أكبرُ، الحمدُ لله الذي ردَّ كيدَه إلى الوسوسَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mmoja wetu anatokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo, akasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi".
Imepokelewa na Abu Daud na Nasai katika AlkubraaDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hutokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo. Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga Takbira mara mbili na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudisha vitimbi vya shetani na kuvigeuza kuwa ni wasiwasi,

Mafunzo
  1. Kumewekwa wazi kuwa Shetani humuwinda muislamu kwa njia ya wasiwasi; ili kumtoa katika imani na kumuingiza katika ukafiri.
  2. Kumewekwa wazi kuwa shetani ni kiumbe dhaifu mbele ya wenye imani, kwani Shetani hawezi kufanya chochote zaidi ya kutia wasiwasi.
  3. Muumini anapasa kuupinga wasiwasi utokanao na shetani na kuuzuia wasiwasi huo.
  4. Ni sheria kuleta Takbira kwenye jambo zuri au lenye kufanana na mambo mazuri.
  5. Ni katika sheria muislamu kumuuliza mtu mjuzi kwa kila jambo linalomtatiza.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 435) (5112) السنن الكبرى للنسائي (9/ 249) (10435)، شرح سنن أبي داود للعباد (580/ 28)، صحيح مسلم (1/ 119) (132)، شرح سنن أبي داود لابن رسلان (19/370)، ومرقاة الصعود (3/1301).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَأْتِي الشَّيْطَانُ أَحَدَكُمْ فَيَقُولُ: مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ حَتَّى يَقُولَ: مَنْ خَلَقَ رَبَّكَ؟ فَإِذَا بَلَغَهُ فَلْيَسْتَعِذْ بِاللهِ وَلْيَنْتَهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu tiba sahihi ya kujiepusha na maswali ambayo Shetani huyatumia kumtia wasiwasi muumini, Basi Shetani husema: Ni nani aliyeumba kitu fulani? Ni nani aliyeumba mbingu? Ni nani aliyeumba Ardhi? Hivyo basi muumini kutokana na dini yake na maumbile yake na akili yake humjibu kwa kusema kuwa ni Mwenyezi Mungu, Lakini Shetani haishii hapo kwenye kutia wasiwasi, bali anahama mpaka anafikia kusema; Ni nani aliyemuumba Mola wako? Basi wakati huo muislamu atajizuilia na wasiwasi huu kwa kufanya mambo matatu: Kwa kumuamini Mwenyezi Mungu. Na kwa kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, Na kuacha kuendekeza wasiwasi.

Mafunzo
  1. Kupinga wasiwasi wa Shetani na hatari zake na kuacha kufikiria wasiwasi, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuondosha wasiwasi.
  2. Kila aina ya wasiwasi unaotokea kwenye moyo wa mwanadamu na unapingana na sheria basi wasiwasi huo ni wa Shetani.
  3. Kumekatazwa kufikiria dhati ya Mwenyezi Mungu, na kuhimizwa kufikiria kuhusu viumbe wa Mwenyezi Mungu na alama zake.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 123) (3276)، صحيح مسلم (1/ 120) (134)، إكمال المعلم (1/432)، المفهم (1/345)، فتح الباري (6/ 340)، طرح التثريب (8/163)، بهجة قلوب الأبرار (ص 27).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 13
Hadithi 13
  1. Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu
  2. , atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo
  3. Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa
  4. Umejengwa uislamu kwa mambo matano
  5. Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni
  6. kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli
  7. Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi
  8. Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo
  9. Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo
  10. Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?
  11. na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri
  12. Umejengwa uislamu kwa mambo matano
  13. Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com