عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «يَقْبِضُ اللَّهُ الأَرْضَ، وَيَطْوِي السَّمَوَاتِ بِيَمِينِهِ، ثُمَّ يَقُولُ: أَنَا المَلِكُ، أَيْنَ مُلُوكُ الأَرْضِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu ataikamata Ardhi na kuikusanya, na ataikunja Mbingu kwa mkono wake wa kulia na aikunjekunje na aiondoe na aimalize, kisha asema: Mimi ndiye Mfalme, wako wapi wafalme wa Ardhini?!
Mafunzo
- Ukumbusho wa kuwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu ndio wenye kubakia, na Ufalme wa asiyekuwa yeye ni wenye kuondoka.
- Utukufu wa Mwenyezi Mungu na Ukubwa wa kudura zake na mamlaka yake na ukamilifu wa Ufalme wake.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 126) (4812)، صحيح مسلم (4/ 2148) (2787)، فتح الباري (13/367)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (23/ 101)، البحر المحيط الثجاج (43/324).