Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza kuapa kwa baba, atakayetaka kuapa basi asiape ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, na wala asiape kwa jina la mwingine. Kisha Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakuwahi tena kuapa tangu alipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akikataza kufanya hivyo, si kwa makusudi wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine aliyeapa kinyume na Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Uharamu wa kuapia kinyume na Mwenyezi Mungu, na kataja kumwapia baba kwa sababu hii ilikuwa ni katika desturi za zama za ujinga.
Kiapo: Ni kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa majina yake au sifa zake katika jambo miongoni mwa mambo kwa ajili kutilia mkazo.
Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake kwa wepesi wake wa kutekeleza na uzuri wa uelewa wake na unyenyekevu wake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 132) (6647).
صحيح مسلم (3/ 1266) (1646).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص684).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 134).
عن عائشة أم المؤمنين وعبد الله بن عباس رضي الله عنهما قالا: لَمَّا نَزَلَ بِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَفِقَ يَطْرَحُ خَمِيصَةً لَهُ عَلَى وَجْهِهِ، فَإِذَا اغْتَمَّ بِهَا كَشَفَهَا عَنْ وَجْهِهِ، فَقَالَ وَهُوَ كَذَلِكَ: «لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى اليَهُودِ وَالنَّصَارَى، اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ» يُحَذِّرُ مَا صَنَعُوا.
Kutoka kwa Aisha na Abdillah bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao wamesema: Yalipomfika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mauti akawa anaweka nguo yake juu ya uso wake, anapozidiwa kupumua anaifunua kutoka usoni kwake, na anasema naye akiwa katika hali hiyo: "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni Misikiti" Akitahadharisha waliyoyafanya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Aisha na bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakuwa kilimpofika kifo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alianza kuweka kipande cha kitambaa juu ya uso wake, akibanwa na pumzi kwa sababu ya kilevi cha kifo anakitoa usoni kwake, akasema akiwa katika hali hiyo mbaya: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Manaswara, na akawafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao walijenga Misikiti juu ya makaburi ya Manabii wao, laiti kama jambo hili lisingekuwa na hatari basi asingelieleza katika sehemu kama hii, kwa sababu hii ameukataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kufanana na kitendo hicho; kwa sababu ni katika vitendo vya Mayahudi na Manaswara, na ni kwa sababu ni njia inayopelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mafunzo
Kukatazwa kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa Misikiti inayoswaliwa kwaajili ya Mwenyezi Mungu, kwasababu hilo ni njia inayopelekea katika ushirikina.
Kipaumbele kikubwa cha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuitilia umuhimu tauhidi na hofu yake juu ya kutukuzwa makaburi; kwa sababu hilo linapelekea katika ushirikina.
Inafaa kuwalaani Mahayudi na Manaswara na atakayefanya mfano wa vitendo vyao ikiwemo kuyajengea makaburi na kuyafanya kuwa mahali pa ibada.
Kujengea makaburi ni katika taratibu za Mayahudi na Manaswara, na katika hadithi hii kuna katazo la kujifananisha nao.
Miongoni mwa kuyafanya makaburi kuwa misikiti ni kuswali hapo au kuswali kwa kuyaelekea, hata kama hapajajengwa msikiti.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 95) (435)، (2/ 102) (1390).
صحيح مسلم (1/ 377) (531)، (1/ 376) (529).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، للشيخ صالح الفوزان (ص170).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي (ص185).
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «قَالَ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ، مَنْ عَمِلَ عَمَلًا أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ».
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.
Mafunzo
Tahadhari ya ushirikina kwa aina zake zote; nakuwa ushirikina huzuia kukubaliwa amali.
Kuleta hisia ya utajiri wa Allah na utukufu wake ni katika mambo yanayosaidia kutakasa matendo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2289) (2985).
شرح النووي على مسلم (18/ 115).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص287).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص325).
Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha mapenzi, kama alichopata Ibrahim -Amani iwe juu yake-, na kwa ajili hiyo alikanusha kuwa na mwandani zaidi ya Allah; Kwa sababu moyo wake umejaa mapenzi ya Allah Mtukufu na kumtukuza kwake na kumtambua kwake, hivyo hauwezi kupata nafasi kwa yeyote zaidi ya Allah, Na lau kama angelijifanyia mwandani katika viumbe basi angelikuwa ni Abubakari. Kisha akatahadharisha kwa kuchupa mipaka inayofaa katika mapenzi kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao na wema wao mpaka wakayageuza kuwa miungu ya kishirikina inayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na wakajenga juu ya makaburi yao misikiti na mahekalu, na akaukataza -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake wasijekufanya mfano vitendo vyao.
Mafunzo
Ubora wa Abubakari -Radhi za Allah ziwe juu yake-, nakuwa yeye ndiye Swahaba bora na mtu bora kwa kuushika ukhalifa wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kifo chake.
Kujenga misikiti juu ya makaburi ni katika maovu ya umma zilizopita.
Katazo la kuyafanya makaburi kuwa sehemu za ibada kwa ajili ya kuswalia hapo au kuyaelekea na kujengwa juu yake misikiti au makuba, kwa tahadhari ya kutoangukia katika ushirikina kwa sababu ya hilo.
Tahadhari ya kuchupa mipaka kwa watu wema, kwani hupelekea kwenye ushirikina.
Uhatari wa yale aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba aliyatilia mkazo kabla ya kifo chake kwa siku tano.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 377) (532).
شرح النووي على مسلم (5/ 13).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص188).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص172).
Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na AhmadDarajaSahihi kwa mkusanyiko wa njia zake
Maelezo
Amekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi Mungu na fulani; Na hii ni kwa sababu matashi ya Mwenyezi Mungu na maamuzi yake ni ya moja kwa moja na hakuna yeyote anaye shirikiana naye, Na katika matumizi ya kiunganishi "Na" hii inamaanisha kuwa kuna mtu anayeshirikiana pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa wako sawa katika maamuzi. Lakini aseme: Akitaka Mwenyezi Mungu, kisha fulani, Hivyo basi afanye matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: " Kisha" badala ya "Na", kwa sababu kiunganishi "Kisha" humaanisha kuja baada ya kitu kingine na kuchelewa pia.
Mafunzo
Uharamu wa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka", na mfano wa matamshi kama haya ambayo yatamaanisha kuunganisha neno na Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "Na"; kwa sababu hii ni katika shirki ya matamshi.
Inafaa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka", na mfano wa hayo ambayo yanamaanisha kuunganisha maneno kwa kiunganishi "Kisha"; kwa kuwa hakuna katazo ndani yake.
Hapa kumethibitishwa matashi kwa Mwenyezi Mungu, na matashi ya mja, nakuwa matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Katazo la kuwashirikisha viumbe katika matashi ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kwa matamshi.
Ikiwa mtu ataitakidi kuwa matashi ya mja ni sawa na matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuenea kwake na kutokuwa na mipaka, nakuwa mja ana matashi binafsi ya kwake mwenyewe, hii ni shirki kubwa, ama akiitakidi kuwa matashi ya mja yanakaribia matashi ya Mwenyezi Mungu; hii ni shirki ndogo.
Marejeo
السنن الكبرى للنسائي (9/ 361) (10755).
سنن أبي داود (7/ 334) (4980).
مسند أحمد (38/ 299) (23265)، (38/ 364) (23339).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص368).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص329).
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: "لأن أحلف بالله كاذبًا أحب إليَّ من أن أحلف بغيره صادقًا".
Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli".
Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah - Imepokelewa na Abdul RazaaqDarajaSahihi
Maelezo
Anasema bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ninasema uongo -tukichukulia kutokea hilo- kunapendeka zaidi kwangu kuliko kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ni mkweli ndani yake; na hii nikuwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwa uongo kumeshinda kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli; kwasababu kuapa kwa Mwenyezi Mungu katika hali hii kuna uzuri wa tauhidi, na kuna ubaya wa dhambi la uongo, na kuapa kwa asiyekuwa yeye kwa ukweli, kuna uzuri wa ukweli na dhambi ya ushirikina, na zuri la tauhidi ni kubwa zaidi kuliko zuri la ukweli, na dhambi la uongo ni jepesi sana kuliko dhambi la ushirikina.
Marejeo
كتاب التوحيد للإمام محمد بن عبد الوهاب ص252 ت: د. دغش العجمي . مكتبة أهل الأثر , الطبعة الخامسة , 1435ه
الجديد في شرح كتاب التوحيد لمحمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي, ت: محمد بن أحمد سيد , مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة، 1424ه
الملخص في شرح كتاب التوحيد للشيخ صالح الفوزان , دار العاصمة , الطبعة الأولى 1422ه
المصنف لابن أبي شيبة, ت: كمال يوسف الحوت, مكتبة الرشد, الطبعة: الأولى، 1409
إرواء الغليل للألباني , المكتب الإسلامي , ط2, 1405ه
Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo yake ambayo ni yake pekee, au kusema kuwa anajua mambo yaliyo jificha, au anastahiki kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, kama walivyofanya Wakristo kwa Issa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- Kisha akaweka wazi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na akaamrisha tuseme kuhusu yeye: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.
Mafunzo
Tahadhari ya kuvuka mpaka wa kisheria katika kuzikuza sifa; kwani hilo hupelekea katika ushirikina.
Aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tayari yamekwisha tokea katika umma huu, kundi likachupa mipaka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kundi kwa watu wa nyumba yake, na kundi kwa mawalii wake (wacha Mungu), wakatumbukia katika ushirikina.
Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye ni mja anaelelewa na Mwenyezi Mungu haifai kuelekezewa chochote katika mambo mahususi ya kiuungu.
Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye katumwa kutoka kwa Allah hivyo, ni wajibu kumsadikisha na kumfuata.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 167) (3445).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري، محمود بن أحمد بدر الدين العيني (16/ 37).
فتح الباري، لابن حجر (6/ 490).
منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، حمزة محمد قاسم (4/ 208).
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Palisemwa ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni mtu gani atakayepata furaha zaidi ya uombezi wako siku ya Kiyama? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilijua kuwa ewe Abuu Huraira hatoniuliza mwingine hadithi hii kabla yako, kwa kile nilichokiona kwako, pupa yako juu ya hadithi, Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).
Mafunzo
Kuthibitisha uombezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Akhera, nakuwa hautokuwa ila kwa watu wa tauhidi.
Uombezi wake -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuomba kwake kupitia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yule atakaye stahiki Moto katika watu wa tauhidi ili asiuingie, na aliyeuingia atoke.
Ubora wa neno la tauhidi lililotakasiwa nia kwa ajili ya Allah Mtukufu na athari zake kubwa.
Kulihakikisha neno la tauhidi kunakuwa kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi makusudio yake kwa namna inavyotakikana.
Ubora wa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na pupa yake juu ya elimu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 31) (99).
منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة محمد قاسم (1/ 197).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 343).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com