Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما: أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَلَّمَهُ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ، فَقَالَ: مَا شَاءَ اللهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ عَدْلًا؟ قُلْ: مَا شَاءَ اللهُ وَحْدَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Imepokelewa na Nasai katika Sunan Alkubra na Ibn Majah na AhmadDarajaUpokezi wake ni mzuri
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.

Mafunzo
  1. Katazo la kusema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka, na mfano wake katika yale yanayounganisha matashi ya mja katika matashi ya Mwenyezi Mungu kwa "na"; kwani hii ni katika shirki ndogo.
  2. Ulazima wa kukemea uovu.
  3. Mtume rehema na amani zimfikie alilinda mipaka ya tauhidi, na akaziba njia za ushirikina.
  4. Wakati wa kuondoa uovu ni vyema kumuelekeza anayefikishiwa ujumbe katika mbadala wa halali, kwa kumuiga Mtume rehema na amani zimfikie.
  5. Kukusanya baina ya kauli yake rehema na amani zimfikie katika hadithi hii: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", na kauli yake katika hadithi nyingine: "Sema: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe" Nikuwa kauli ya mtu: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe", hii inafaa, lakini kauli ya: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake" ndio bora zaidi.
  6. Inafaa kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka" lakini bora zaidi ni kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Marejeo

السنن الكبرى للنسائي (9/ 362) (10759). سنن ابن ماجه (3/ 252) (2117). مسند أحمد (5/ 297) (3247). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص373). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص335). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 230).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com