Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda kwa mwingine pasina kadari ya Mwenyezi Mungu, nikuwa madai hayo ni batili, nakuwa mikosi ya ndege ni batili, nayo ni mikosi kupitia kitu chochote chenye kuhisika au kuonekana, kama ndege au wanyama, au walemavu, au namba au siku au kinginecho, hapa ametaja ndege kwa sababu ni kitendo kilichokuwa maarufu zama za ujinga, na asili yake ilikuwa ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi yoyote, kama safari au biashara au kinginecho, akiruka kuelekea kushoto mtu anaamini ni mkosi, na anaahirisha alichotaka kukifanya. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa anafurahishwa sana na mtu kujipa matumaini, nayo ni mtu kuwa na furaha na raha, kwa maneno mazuri anayoyasikia, yatakayomfanya awe na dhana nzuri na Mola wake Mlezi.
- Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hakuna awezaye kuleta kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna awezaye kuzia shari isipokuwa Mwenyezi Mungu.
- Katazo la kuamini mikosi ya ndege, nayo ni kila kitu kinachoaminika kuwa ni mkosi, na kufanya kazi isifanyike.
- Matumaini si katika mikosi iliyokatazwa, bali ni katika kumdhania kheri Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kila kitu kinachotokea ni kwa mipango na makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, yeye pekee asiye na mshirika wake.
صحيح البخاري (7/ 135) (5756). صحيح مسلم (4/ 1746) (2224). فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (ص310). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 570). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص230). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص255). التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص333).