Amesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Uharamu wa kujenga Misikiti juu ya makaburi, au kuswali hapo, au kuzika maiti ndani ya msikiti; hii ikiwa ni kuziba njia za kuelekea katika ushirikina.
- Kujenga Misikiti juu ya makaburi, na kutundika picha, hiki ni kitendo cha Mayahudi, nakuwa mwenye kufanya hivi atakuwa kafanana nao.
- Uharamu wa kutengeneza picha za viumbe hai (wenye roho).
- Atakayejenga msikiti juu ya kaburi na akachoro ndani yake picha, huyu ni katika viumbe waovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Sheria imeuhami sana upande wa tauhidi kwa himaya iliyokamilika, kwa kuziba njia zote ambazo zinaweza kusababisha kufika katika ushirikina.
- Katazo la kuchupa mipaka kwa watu wema; kwani ni sababu ya kuingia katika shirki.
صحيح البخاري (1/ 94) (434). صحيح مسلم (1/ 375) (528). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (7/ 2857). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 115). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 598). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 469). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص290). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص183). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص168).