عن أبي مَرْثَدٍ الغَنَوِيّ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ، وَلَا تُصَلُّوا إِلَيْهَا».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.
Mafunzo
- Katazo la kusali makaburini au kati kati yake au kuyaelekea, isipokuwa swala ya jeneza kama ilivyothibiti katika mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Katazo la kusali kwa kuyaelekea makaburi ni kuziba mianya ya kuingia katika ushirikina.
- Uislamu umekataa kuchupa mipaka katika makaburi na kuyadhalilisha pia, hakuna kuyapuuza wala kuyatukuza.
- Heshima ya muislamu inabakia hata baada ya kufa kwake, kwa kauli yake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai".
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 668) (972). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 30). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لمحمد العثيمين (1/ 522). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 285).