Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha

عَنْ عَبْدَ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عَنْهُمَا يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا لَمْ تَضُرَّهُ مَعَهُ خَطِيئَةٌ، وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ يُشْرِكُ بِهِ لَمْ يَنْفَعْهُ مَعَهُ حَسَنَةٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.

Mafunzo
  1. Tahadhari dhidi ya ushirikina, na kwamba hilo ni katika madhambi na makosa makubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu haisamehe.
  2. Fadhila ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kwamba hilo linawajibisha kuingia Peponi; hata ikiwa baada ya kuadhibiwa.
  3. Umuhimu wa kudumu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu mpaka kufa, na kutofanya kinyume chake ambacho ni ushirikina.
Marejeo

مسند أحمد (11/ 155- 156) (11/ 157) (6586). فيض القدير شرح الجامع الصغير (6/220).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com