Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.
Mafunzo
Ubora wa Tauhidi na kuwa yeyote atakaye kufa hali yakuwa ni muumini wa kweli hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi.
Hatari ya ushirikina, nakuwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni.
Wafanya maasi wale wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 94) (93)، إكمال المعلم بفوائد مسلم (1/ 363)، شرح النووي على مسلم (2/96) المفهم للقرطبي (1/290)، تطريز رياض الصالحين (ص 281)، الكوكب الوهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج (3/63).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com