Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ: لَوْ أَنَّ لَكَ مَا فِي الأَرْضِ مِنْ شَيْءٍ أَكُنْتَ تَفْتَدِي بِهِ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ: أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا، وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَلّاَ تُشْرِكَ بِي شَيْئًا، فَأَبَيْتَ إِلَّا أَنْ تُشْرِكَ بِي».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio, atasema: Nilikutakeni jambo jepesi zaidi kuliko hili, nanyi mkiwa katika mgongo wa Adam: yakuwa msinishirikishe na chochote, mkakataa isipokuwa kunishirikisha na chochote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.

Mafunzo
  1. Thamani ya tauhidi na wepesi wa kuifanyia kazi.
  2. Hatari ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine na mwisho wake mbaya.
  3. Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa wanadam wote wakiwa katika mgongo wa baba yao Adam ya kutomshirikisha.
  4. Tahadhari ya ushirikina nakuwa thamani ya dunia yote haiwezi kumsaidia chochote kafiri siku ya Kiyama.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 115) (6557). صحيح مسلم (4/ 2160) (2805). عمدة القاري شرح صحيح البخاري، لبدر الدين العيني (15/ 213). معجم اللغة العربية المعاصرة، لأحمد مختار(2/ 1311). معارج القبول بشرح سلم الوصول إلى علم الأصول، لحافظ الحكمي (1/ 96).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com