Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَقُولُوا: مَا شَاءَ اللهُ وَشَاءَ فُلَانٌ، وَلَكِنْ قُولُوا: مَا شَاءَ اللهُ ثُمَّ شَاءَ فُلَانٌ».
Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na AhmadDarajaSahihi kwa mkusanyiko wa njia zake
Maelezo

Amekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi Mungu na fulani; Na hii ni kwa sababu matashi ya Mwenyezi Mungu na maamuzi yake ni ya moja kwa moja na hakuna yeyote anaye shirikiana naye, Na katika matumizi ya kiunganishi "Na" hii inamaanisha kuwa kuna mtu anayeshirikiana pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa wako sawa katika maamuzi. Lakini aseme: Akitaka Mwenyezi Mungu, kisha fulani, Hivyo basi afanye matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: " Kisha" badala ya "Na", kwa sababu kiunganishi "Kisha" humaanisha kuja baada ya kitu kingine na kuchelewa pia.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka", na mfano wa matamshi kama haya ambayo yatamaanisha kuunganisha neno na Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "Na"; kwa sababu hii ni katika shirki ya matamshi.
  2. Inafaa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka", na mfano wa hayo ambayo yanamaanisha kuunganisha maneno kwa kiunganishi "Kisha"; kwa kuwa hakuna katazo ndani yake.
  3. Hapa kumethibitishwa matashi kwa Mwenyezi Mungu, na matashi ya mja, nakuwa matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Katazo la kuwashirikisha viumbe katika matashi ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kwa matamshi.
  5. Ikiwa mtu ataitakidi kuwa matashi ya mja ni sawa na matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuenea kwake na kutokuwa na mipaka, nakuwa mja ana matashi binafsi ya kwake mwenyewe, hii ni shirki kubwa, ama akiitakidi kuwa matashi ya mja yanakaribia matashi ya Mwenyezi Mungu; hii ni shirki ndogo.
Marejeo

السنن الكبرى للنسائي (9/ 361) (10755). سنن أبي داود (7/ 334) (4980). مسند أحمد (38/ 299) (23265)، (38/ 364) (23339). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص368). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص329).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com