Ametaja Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii madhambi ambayo yanazingatiwa kuwa ni katika madhambi makubwa, nayo: ni kuwekewa Mwenyezi Mungu Mtukufu mshirika katika uumbaji wake na kuabudiwa kwake, na ameanza na hili, kwasababu ndiyo dhambi kubwa kuliko yote, na kukata matarajio na matumaini kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu huko ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu na ni kutojua upana wa rehema zake, na kujiaminisha kwa kumvuta taratibu mja kwa kumpa neema ili mpaka aje kumchukua akiwa kaghafilika, na si makusudio ya hadithi kudhibiti idadi ya madhambi makubwa kuwa hakuna zaidi ya haya yaliyotajwa, lakini makusudio yake ni kubainisha makubwa yake.
- Kugawanyika kwa madhambi makubwa na madogo
- Nikuwa ushirikina ni dhambi kubwa na ni kosa kubwa kuliko yote.
- Uharamu wa kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu Mtukufu- na kukata tamaa na rehema zake, nakuwa hayo ni katika madhambi makubwa.
- Kufaa kumsifu Mwenyezi Mungu kwa vitimbi katika kupambana na wenye vitimbi, na hii ni sifa ya ukamilifu, na sifa mbaya ni vitimbi kwa asiyestahiki kufanyiwa vitimbi.
- Nikuwa la msingi kwa mja awe kati ya hofu na kutaraji, akiwa na hofu hawezi kukata tamaa, na akitaraji hawezi kujiaminisha.
- Kuthibitisha sifa ya huruma kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
- Ulazima wa kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu Mtukufu.
كتاب التوحيد، محمد بن عبد الوهاب، تحقيق: دغش العجمي، مكتبة أهل الأثر، الطبعة: الخامسة 1435هـ. الجديد في شرح كتاب التوحيد، محمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي، تحقيق: محمد بن أحمد سيد، مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة 1424هـ، 2003م. الملخص في شرح كتاب التوحيد، صالح بن فوزان بن عبد الله الفوزان، دار العاصمة، الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ، 2001م. جامع معمر بن راشد، معمر بن أبي عمرو راشد الأزدي، نزيل اليمن، تحقيق: حبيب الرحمن الأعظمي، الناشر: المجلس العلمي بباكستان، وتوزيع المكتب الإسلامي ببيروت، الطبعة: الثانية 1403 هـ.