Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho

عن عبد الله بن عكيم رضي الله عنه مرفوعاً: «مَنْ تَعَلَّقَ شيئا وُكِلَ إليه».
Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri
Maelezo

Atakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.

Mafunzo
  1. Katazo la kuegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Ulazima wa kuegemea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
  3. Kubainishwa madhara ya ushirikina na ubaya wa mwisho wake.
  4. Malipo huendana na matendo.
  5. Nikuwa malipo ya kitendo hurudi kwa mfanyaji yakiwa ya kheri au ya shari.
  6. Kushindwa kwa mwenye kujiondoa kwa Mwenyezi Mungu na akatafuta manufaa kwa asiyekuwa yeye.
Marejeo

الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ- 2001م. الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م. مسند الإمام أحمد بن حنبل، تحقيق: شعيب الأرنؤوط - عادل مرشد، وآخرون، نشر: مؤسسة الرسالة، الطبعة: الأولى، 1421هـ - 2001م. سنن الترمذي، نشر: شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي – مصر، الطبعة: الثانية، 1395هـ - 1975م. غاية المرام في تخريج أحاديث الحلال والحرام، للألباني، المكتب الإسلامي - بيروت، الطبعة: الثالثة - 1405.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com