Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.
- Ibada hazielekezwi ila kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee.
- Ubora wa tauhidi, nakuwa atakayekufa katika tauhidi ataingia peponi, hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake.
- Hatari ya ushirikina, nakuwa atakayekufa katika ushirikina ataingia motoni.
صحيح البخاري (6/ 23) (4497). صحيح مسلم (1/ 94) (92). فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (ص76). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 120). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص47). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص59). التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص42).