Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَأْتِي الشَّيْطَانُ أَحَدَكُمْ فَيَقُولُ: مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ حَتَّى يَقُولَ: مَنْ خَلَقَ رَبَّكَ؟ فَإِذَا بَلَغَهُ فَلْيَسْتَعِذْ بِاللهِ وَلْيَنْتَهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu tiba sahihi ya kujiepusha na maswali ambayo Shetani huyatumia kumtia wasiwasi muumini, Basi Shetani husema: Ni nani aliyeumba kitu fulani? Ni nani aliyeumba mbingu? Ni nani aliyeumba Ardhi? Hivyo basi muumini kutokana na dini yake na maumbile yake na akili yake humjibu kwa kusema kuwa ni Mwenyezi Mungu, Lakini Shetani haishii hapo kwenye kutia wasiwasi, bali anahama mpaka anafikia kusema; Ni nani aliyemuumba Mola wako? Basi wakati huo muislamu atajizuilia na wasiwasi huu kwa kufanya mambo matatu: Kwa kumuamini Mwenyezi Mungu. Na kwa kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, Na kuacha kuendekeza wasiwasi.

Mafunzo
  1. Kupinga wasiwasi wa Shetani na hatari zake na kuacha kufikiria wasiwasi, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuondosha wasiwasi.
  2. Kila aina ya wasiwasi unaotokea kwenye moyo wa mwanadamu na unapingana na sheria basi wasiwasi huo ni wa Shetani.
  3. Kumekatazwa kufikiria dhati ya Mwenyezi Mungu, na kuhimizwa kufikiria kuhusu viumbe wa Mwenyezi Mungu na alama zake.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 123) (3276)، صحيح مسلم (1/ 120) (134)، إكمال المعلم (1/432)، المفهم (1/345)، فتح الباري (6/ 340)، طرح التثريب (8/163)، بهجة قلوب الأبرار (ص 27).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com