Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

Hadithi 29

Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: قال رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللهَ يَغَارُ، وَإِنَّ الْمُؤْمِنَ يَغَارُ، وَغَيْرَةُ اللهِ أَنْ يَأْتِيَ الْمُؤْمِنُ مَا حَرَّمَ عَلَيْهِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu hupata wivu na huchukia na hukarahika, kama ambavyo muumini hupata wivu na huchukia na kukarahika, nakuwa sababu ya wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa machafu kama zinaa liwati (Ushoga na ubasha) wizi na kunywa pombe na mengineyo katika machafu.

Mafunzo
  1. Kutahadhari na hasira na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake pale yanapofanywa maharamisho yake.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 35) (5223). صحيح مسلم (4/ 2114) (2761). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص62). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 496). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 96). صفات الله عز وجل الواردة في الكتاب والسنة، لعلوي السَّقَّاف (ص267).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza

عن ابن عباس رضي الله عنهما أنه رأى رجلا انْتَفَضَ لما سمع حديثا عن النبي صلى الله عليه وسلم في الصفات -استنكارا لذلك– فقال: "ما فَرَقُ هؤلاء؟ يجدون رِقَّةً عند مُحْكَمِهِ، ويَهْلِكُونَ عند مُتَشَابِهِهِ" .
Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba yeye alimuona mtu alishituka aliposikia mazungumzo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika sifa (za Allah) -akafanya kama ishara ya kulipinga hilo- akasema: "Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza".
Imepokelewa naIbn Abii A'swim - Imepokelewa na Abdul RazaaqDarajaSahihi
Maelezo

Anawakemea bin Abbasi watu miongoni mwa wale waliohudhuria kikao chake katika watu wa kawaida wanaopatwa na hofu pale wanaposikia chochote katika hadithi za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu sifa, na wanatikisika kama ishara ya kulipinga hilo, haijapatikana kwao imani ya wajibu kwa yale yaliyothibiti toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wakajua maana yake kutoka ndani ya Qur'ani ambayo muumini hawezi kuwa na shaka, na baadhi yao huzichukulia katika maana isiyokuwa yake aliyoitaka Mwenyezi Mungu wakaangamia kwa hilo.

Marejeo

كتاب التوحيد للإمام محمد بن عبد الوهاب ص252 ت: د. دغش العجمي . مكتبة أهل الأثر , الطبعة الخامسة , 1435ه الجديد في شرح كتاب التوحيد لمحمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي, ت: محمد بن أحمد سيد , مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة، 1424ه الملخص في شرح كتاب التوحيد للشيخ صالح الفوزان , دار العاصمة , الطبعة الأولى 1422ه كتاب السنة لابن أبي عاصم ومعه ظلال الجنة للألباني, المكتب الإسلامي, ط4 1419

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قَارِبُوا وَسَدِّدُوا، وَاعْلَمُوا أَنَّهُ لَنْ يَنْجُوَ أَحَدٌ مِنْكُمْ بِعَمَلِهِ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَلَا أَنْتَ؟ قَالَ: «وَلَا أَنَا، إِلَّا أَنْ يَتَغَمَّدَنِيَ اللهُ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَفَضْلٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kufanya amali njema, na wamche Mwenyezi Mungu kadiri wawezavyo, pasina kuchupa mipaka wala uzembe, na wakusudie katika amali zao kupatia kwa kuwa na ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amali zao zikubaliwe, ili iwe ni sababu ya kuteremka kwa rehema juu yao. Kisha akawaeleza kuwa amali hazitomuokoa yeyote miongoni mwao kamwe; bali ni lazima kuwe na rehema ya Mwenyezi Mungu. Wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hazitokuokoa amali zako pamoja na ukubwa wa kiwango chake? Akasema: Hata mimi, ila kama atanisitiri Mwenyezi Mungu kwa fadhila na rehema zake.

Mafunzo
  1. Amesema Imam Nawawi: (Fanyeni na mjiweke karibu): Yaani tafuteni usawa, na muufanyie kazi, na mkishindwa kuupata basi, jiwekeni karibu; yaani jiwekeni karibu nao, na usawa: Ni kupatia, nako nikuwa kati ya kuchupa mipaka na uzembe, msichupe mipaka wala msifanye uzembe.
  2. Amesema bin Bazi: Matendo mema ndio sababu ya kuingia peponi, kama ambavyo matendo machafu ni sababu ya kuingia motoni, na hadithi inabainisha kuwa kuingia peponi si tu kwa kufanya matendo pekee, bali ni lazima kuwe na msamaha wa Mwenyezi Mungu na rehema yake Aliyetakasika na kutukuka, hivyo kuingia kwao ni kwa sababu ya matendo yao, lakini kinachowajibisha hilo ni rehema yake Mtukufu, na msamaha wake na maghufira yake.
  3. Mja ahadaiki na kujifaharisha kwa matendo yake vyovyote vile yatavyofikia; kwa sababu haki ya Mwenyezi Mungu ni kubwa kuliko amali yake, ni lazima amali iwe na hofu na kutaraji rehema, vyote kwa pamoja.
  4. Fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake kwa waja wake ni pana kuliko amali zao.
  5. Matendo mema ni sababu ya kuingia peponi, na kufuzu kuipata ni kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema kutoka kwake.
  6. Amesema Al-Karmaani: "Ikiwa watu wote hawatoingia peponi ila kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, hivyo namna ya kumhusisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kumtaja kuwa hatoingia peponi ila kwa rehema ya Mwenyezi Mungu pamoja nakuwa kapewa uhakika wa kuingia peponi, hii inamaanisha kuwa mtu mwingine asiyekuwa yeye ndio ana haki zaidi ya kutoingia ila kwa rehema yake Mwenyezi Mungu.
  7. Amesema Imam Nawawi: Katika maana ya kauli yake Mtukufu: "Ingieni peponi kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [An Nahl: 32], "Na hiyo pepo mliyorithishwa ni kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Az-Zukhruf: 72] Na mifano mingine ya aya kama hizi zinazoonyesha kuwa matendo yatampeleka mtu peponi, hazipingani na hadithi hii, bali maana ya aya hizi nikuwa kuingia peponi ni kwa sababu ya matendo kisha kupata taufiki ya matendo hayo, na kuongozwa katika Ikhlasi ndani yake, na kukubalika kwake ni kwa rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na fadhila zake, hapa itakubalika kusema kuwa mtu hajaingia peponi kwa matendo pekee, na inasihi kusema kuwa kaingia kwa matendo: Yaani kwa sababu yake, nayo pia ni katika rehema.
  8. Amesema bin Jauzi: Hapa yanapatikana majibu manne: La kwanza: Nikuwa kupata taufiki ya kutenda amali njema ni katika rehema za Mwenyezi Mungu, na lau kama si rehema za Mwenyezi Mungu zilizotangulia isingepatikana imani wala utiifu ambao ndio sababu ya kuokoka. La pili: Nikuwa manufaa ya mtumwa yapo kwa bosi wake hivyo matendo yake ni haki stahiki ya bwana wake, vyovyote vile atakavyomneemesha kwa malipo yote hayo ni katika fadhila zake. La tatu: Imekuja katika baadhi ya hadithi kuwa hata kuingia pepo kwenyewe pia ni katika rehema za Mwenyezi Mungu, na mgawanyo wa madaraja utakuwa kwa mujibu wa matendo. La nne: Nikuwa matendo ya utiifu yalikuwa kwa muda mfupi, na thawabu hazimaliziki, kuneemeshwa ambako hakumaliziki kupitia matendo yanayomalizika hii ni kwa sababu ya fadhila wala si kwa kulinganisha na matendo.
  9. Amesema Ar-Raafii: Nikuwa, mfanyaji hatakiwi kubweteka katika amali zake katika kutafuta kusalimika na kuzipata daraja za juu; kwa sababu alifanya mema kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu na aliacha maasi kwa hifadhi ya Mwenyezi Mungu, yote ni kwa fadhila zake na rehema zake.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 121) (5673). صحيح مسلم (4/ 2170) (2816). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 165). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 321). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 573). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 130).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَقُولُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي، وَأَنَا مَعَهُ حِينَ يَذْكُرُنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُ، وَإِنِ اقْتَرَبَ إِلَيَّ شِبْرًا، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنِ اقْتَرَبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا، اقْتَرَبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja, atakaponitaja ndani ya nafsi yake nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu, na akinitaja katika umati nami nitamtaja katika umati bora kuliko huo, na akisogea kwangu shibri (futi) moja na mimi ninasogea karibu naye kwa mita nzima, na akisogea kwangu kwa mita moja mimi ninasogea kwake kwa zaidi ya mita moja (Baa'a) na akinijia kwa kutembea basi mimi nitamjia kwa mchakamchaka"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, nitampeleka mja wangu kulingana na dhana yake kwangu na hii ni kwa kutaraji mazuri na kutaraji msamaha, na nitamfanyia yote anayoyataraji kutoka kwangu katika mambo ya kheri au mengineyo; na mimi niko pamoja naye kwa kumhurumia na kumuwezesha na kumuongoza na kumlea na kumuunga mkono pindi anaponitaja. Akinitaja ndani ya nafsi yake akiwa peke yake amejitenga kwa kunisabihi na kunitukuza au kwa kinginecho; basi nami nitamtaja ndani ya nafsi yangu. Na akinitaja katika kundi la watu; basi nami nitamtaja katika kundi kubwa na zuri kuliko hilo. Na atakayesogea kwa Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha shibri (futi) moja basi Mwenyezi Mungu humzidishia na kuzidi kujiweka karibu zaidi kwa kiasi cha dhiraa (mita). Na akijiweka karibu naye kwa kiasi cha dhiraa (mita) anajiweka naye kwa kiasi cha zaidi ya mita moja (Baa'a). Na akija kwa Mwenyezi Mungu akiwa anatembea Yeye anamjia kwa mchakamchaka. Mja atakapojiweka karibu na Mola wake Mlezi kwa kumtii na kuelekea kwake, basi Mola Mlezi Mtukufu humzidishia ukaribu ikiwa ni malipo kulingana na amali yake. Kila unapozidi kukamilika uja (utumwa) wa muumini kwa Mola wake Mlezi Mwenyezi Mungu Mtukufu hujiweka karibu naye, hivyo, kipawa cha Mwenyezi Mungu na thawabu zake ni nyingi kuliko amali za mja na tabu zake, na uhalisia nikuwa thawabu za Mwenyezi Mungu ni nyingi kuliko amali kwa kutazama namna na wingi wake. Muumini huwa na dhana nzuri, na kutenda mema, na kwenda mbio na kuzidisha mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Hadithi hii ni katika yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake, na huitwa Hadithil Qudsi, au Hadithil ilaahi, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina mambo maalumu kama ya Qur'ani ambayo inajitofautisha na maneno mengine, kama kisomo chake kutumika kama ibada, na kujitwaharisha kwa ajili yake, na kutoa changamoto, na maswala ya kisayansi na mengineyo.
  2. Amesema Al-Ajurri: Hakika wanaofuata haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyojisifu kwayo Mtukufu, na kwa yale aliyomsifu kwayo mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa yale waliyomsifu kwayo Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale waliofuata muongozo na wala hawakuzua. Mwisho. Wanaofuata Sunna (Ahlus Sunna) wanamthibitishia Mwenyezi Mungu yale aliyoyathibitisha yeye mwenyewe juu ya nafsi yake miongoni mwa majina na sifa, pasina kupotosha wala kukanusha, wala kuuliza namna yake, wala kupiga mfano, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha yeye mwenyewe juu ya nafsi yake, na wananyamaza katika yale ambayo haukuja uthibitisho wala kanusho, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna chochote mfano wake, naye ni msikivu Mwenye kuona".
  3. Kumdhania Allah vizuri ni lazima kuambatane na matendo, amesema Al-Hassan Al-Basari: Hakika muumini alimdhania vizuri Mola wake hivyo akafanya matendo mazuri, na hakika muovu alimdhania vibaya Mola wake kwa hivyo akafanya matendo maovu.
  4. Amesema Qurtubi: Inasemekana kuwa: Maana ya "Dhana ya mja wangu kwangu" ni dhana ya kujibiwa wakati wa kuomba dua, na dhana ya kukubaliwa wakati wa kuomba toba, na dhana ya kusamehewa wakati wa kuomba msamaha, na dhana ya kulipwa wakati wa kufanya ibada kwa sharti zake kwa kushikamana na ahadi za kweli, na ndio mana ni lazima kwa kila mtu ajitahidi kuyasimamia yale aliyo na yakini nayo kuwa hakika Mwenyezi Mungu atamkubalia na atamsamehe; kwa sababu yeye mwenyewe aliahidi hivyo na yeye haendi kinyume na ahadi, akiitakidi au kudhani kuwa Mwenyezi Mungu hatomkubalia nakuwa hayo hayatomnufaisha, huku ndiko kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu ambako ni katika madhambi makubwa, na atakayekufa katika hali hiyo atawakilishwa katika kile alichodhania kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya za hadithi iliyotajwa, "Basi mja wangu na anidhanie mimi akatavyo" anasema: Na ama dhana ya kusamehewa ikiwa ni pamoja na mtu kuendelea na madhambi huo ndio ujinga halisi na ni kujidanganya.
  5. Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu ndani ya nafsi yako na kwa ulimi wako vyote kwa pamoja, yaani mtu ndani ya nafsi yake na moyo wake amuogope Mwenyezi Mungu na akumbuke utukufu wake na haki zake na awe na matarajio kwake na amtukuze na ampende na amdhanie vizuri na amtakasie matendo, na atamke kwa ulimi: Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu) Al-hamdulillaah (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, na Laa ilaaha illa llaah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), Allaahu Akbaru (Mwenyezi Mungu Mkubwa), Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah (Hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu).
  6. Amesema bin Abii Hamza: Atakayemtaja akiwa na hofu basi atampa amani, au akiwa mpweke basi atamfariji.
  7. Shibri: Ni urefu wa kuanzia kidole cha mwisho mpaka kidole gumba wakati wa kukunjua kiganja, na Dhiraa: Ni urefu wa kuanzia ncha yakidole cha kati mpaka katika mfupa wa kiwiko, na Baa'a: Ni urefu wa dhiraa mbili za mtu na muundi wake na upana wa kifua chake; ambayo ni kiasi cha Dhiraa nne.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 121) (7405). صحيح مسلم (4/ 2067) (2675). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 151). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 516). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، حمزة محمد (5/ 372). الجواب الكافي لمن سأل عن الدواء الشافي أو الداء والدواء (ص25). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 510). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 983).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَسْتُرُ عَبْدٌ عَبْدًا فِي الدُّنْيَا إِلَّا سَتَرَهُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu hatomsitiri ndugu yake katika jambo miongoni mwa mambo, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiyama; kwani malipo huendana na matendo, na stara ya Mwenyezi Mungu kwake inakuwa kwa kuzisitiri aibu zake na maasi yake kwa kutoyatangaza mbele ya umati wa siku ya Kiyama, na huenda inawezakuwa kwa kutoyahesabu na kutomkumbusha.

Mafunzo
  1. Sheria ya kumsitiri muislamu anapofanya maasi, pamoja na kumkemea, na kumnasihi, na kumhofisha kwa Mwenyezi Mungu, ama akiwa ni katika watu wa shari na uovu wenye kutangaza wazi maasi na uovu, hawa haitakiwi kusitiriwa; kwa sababu kuwasitiri kunawapa ujasiri wa kufanya maasi, bali wanatakiwa kushitakiwa katika mamlaka husika, hata kama watatajwa kwa majina; kwa sababu mtu anakuwa katangaza wazi yeye mwenyewe maovu yake na maasi yake.
  2. Himizo la kusitiri aibu za watu wengine.
  3. Miongoni mwa faida za kusitiri: Ni kumpa fursa mkosefu ya kuirejea nafsi yake na atubie kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu kutangaza aibu na fedhehe ni katika kueneza maovu, na kunaharibu hali ya hewa ya jamii, na kunawahadaa watu kuendelea kuyatenda.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2002) (2590). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 329). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 255). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 533). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 14).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إِلَّا طَيِّبًا، وَإِنَّ اللهَ أَمَرَ الْمُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ الْمُرْسَلِينَ، فَقَالَ: {يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا، إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ} [المؤمنون: 51] وَقَالَ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ} [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أَشْعَثَ أَغْبَرَ، يَمُدُّ يَدَيْهِ إِلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ، يَا رَبِّ، وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ، وَغُذِيَ بِالْحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ؟».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni". Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo: Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo. Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika. Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua. Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu! Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!

Mafunzo
  1. Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.
  2. Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.
  4. Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.
  5. Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.
  6. Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.
  7. Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 703) (1015). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص27). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص141). الأحاديث الأربعين النووية مع ما زاد عليها ابن رجب وعليها الشرح الموجز المفيد (ص22).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja

عن ابن عباس رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَالَ: قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ، ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ، إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani watayaandika: Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k. Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umma huu katika kuzidishiwa mema na kuandikwa kwake, na kutozidishwa maovu.
  2. Umuhimu wa nia katika amali zote na athari yake.
  3. Fadhila za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- na upole wake na ihisani yake nikuwa mwenye kudhamiria jema na akawa hakulifanya Allah huliandika jema kamili.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 103) (6491). صحيح مسلم (1/ 118) (131). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص85). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص368). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص125). فتح الباري، لابن حجر (11/ 324).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللهَ لَا يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hatazami sura za waja na miili yao, je ni nzuri au mbaya? Je ni mikubwa au midogo? Ina afya au maradhi? Na wala hatazami katika mali zao, je ni nyingi au kidogo? Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka hawaadhibu waja wake wala hawahesabu kwa mambo haya na kutofautiana kwao, lakini anatazama katika nyoyo zao na yale yaliyomo ndani miongoni mwa uchamungu na yakini, na ukweli na ikhlaswi, au ni lengo la kujionyesha au kutaka kusikika, na anatazama katika matendo yao upande wa usahihi wake au kuharibika kwake; Hapo atatoa thawabu na malipo kwa hayo.

Mafunzo
  1. Kuwa na jukumu kubwa la kuirekebisha nafsi, na kuisafisha kutokana na kila sifa mbaya.
  2. Moyo hutengemaa kwa Ikhlaswi, na matendo hutengemaa kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na sehemu hizi mbili ndio mahali pa kutazamwa na kuzingatiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Mwanadamu asidanganyike kwa mali yake wala kwa uzuri wake wala kwa mwili wake wala kwa chochote miongoni mwa mionekano ya dunia.
  4. Tahadhari ya kuridhika na mionekano, na kutorekebisha ndani ya moyo.
Marejeo

صحيح مسلم (2564) (4/ 1986). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 40). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص14). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 25).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 29
Hadithi 29
  1. Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake
  2. Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza
  3. Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake
  4. Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja
  5. Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama
  6. Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii
  7. Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja
  8. Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu
  9. Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya Nafsi yangu na nikaifanya kuwa ni haramu baina yenu, basi msidhulumiane
  10. Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake
  11. “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali
  12. Hakika kwako wewe kuna mambo mawili anayapenda sana Mwenyezi Mungu: Upole, na utaratibu
  13. Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi
  14. kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo
  15. Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake
  16. Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja humuita Jibril na husema: Hakika mimi ninampenda fulani basi mpende, anasema: Jibril humpenda
  17. Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah)
  18. Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni
  19. alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa
  20. “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako?
  21. Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake
  22. Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku
  23. Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera
  24. Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?
  25. Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?
  26. Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala
  27. Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii
  28. Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na maovu, kisha akalibainisha hilo
  29. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko kile nilichomfaradhishia

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com