Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللهَ لَا يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hatazami sura za waja na miili yao, je ni nzuri au mbaya? Je ni mikubwa au midogo? Ina afya au maradhi? Na wala hatazami katika mali zao, je ni nyingi au kidogo? Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka hawaadhibu waja wake wala hawahesabu kwa mambo haya na kutofautiana kwao, lakini anatazama katika nyoyo zao na yale yaliyomo ndani miongoni mwa uchamungu na yakini, na ukweli na ikhlaswi, au ni lengo la kujionyesha au kutaka kusikika, na anatazama katika matendo yao upande wa usahihi wake au kuharibika kwake; Hapo atatoa thawabu na malipo kwa hayo.

Mafunzo
  1. Kuwa na jukumu kubwa la kuirekebisha nafsi, na kuisafisha kutokana na kila sifa mbaya.
  2. Moyo hutengemaa kwa Ikhlaswi, na matendo hutengemaa kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na sehemu hizi mbili ndio mahali pa kutazamwa na kuzingatiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Mwanadamu asidanganyike kwa mali yake wala kwa uzuri wake wala kwa mwili wake wala kwa chochote miongoni mwa mionekano ya dunia.
  4. Tahadhari ya kuridhika na mionekano, na kutorekebisha ndani ya moyo.
Marejeo

صحيح مسلم (2564) (4/ 1986). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 40). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص14). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 25).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com