Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja

عن ابن عباس رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَالَ: قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ، ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ، إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ لَهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani watayaandika: Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k. Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umma huu katika kuzidishiwa mema na kuandikwa kwake, na kutozidishwa maovu.
  2. Umuhimu wa nia katika amali zote na athari yake.
  3. Fadhila za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- na upole wake na ihisani yake nikuwa mwenye kudhamiria jema na akawa hakulifanya Allah huliandika jema kamili.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 103) (6491). صحيح مسلم (1/ 118) (131). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص85). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص368). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص125). فتح الباري، لابن حجر (11/ 324).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com