Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Utukufu wa misikiti na heshima yake; kwa sababu ni nyumba ambazo hutajwa ndani yake jina la Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Himizo la kudumu kuwa msikitini, na wingi kwenda ndani yake, kwa kutafuta mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na radhi zake, na kupunguza kuzunguka masokoni, isipokuwa kwa haja maalumu; kwa kujiepusha kuingia katika sababu za hasira ya Mwenyezi Mungu.
Amesema Nawawi: Misikiti ni mahali pa kushuka rehema na masoko ni kinyume chake.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 464) (671).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1250).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 305).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 655).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (21/ 526).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com