Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu anapompenda mja muumini; mwenye kutii amri zake mwenye kujiepusha na makatazo yake humuita Jibril: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda fulani basi mpende. Basi bwana wa Malaika, Jibril amani iwe juu yake humpenda, basi Jibril hunadi kwa Malaika walioko mbinguni. Hakika Mola wenu anampenda fulani basi nanyi mpendeni, basi humpenda wakazi wa mbinguni, kisha anapewa kukubalika katika nyoyo za waumini kwa kumpenda na kuvutiwa naye na kumridhia. Na anapomchukia Mwenyezi Mungu mja humuita Jibril: Hakika mimi ninamchukia fulani basi mchukie; Basi Jibril humchukia, kisha ananadi Jibril kwa wakazi wa mbinguni: Hakika Mola wenu Mlezi anamchukia fulani basi mchukieni; wanamchukia, kisha anawekewa kuchukiwa na kutofurahiwa ndani ya nyoyo za waumini.
- Amesema Abuu Mohammad Abuu Jamra: Na katika kutanguliza amri katika hilo ya kumuamrisha Jibril kabla ya Malaika wengine ni kuonyesha utukufu wa nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko Malaika wengine miongoni mwao.
- Atakayependwa na Mwenyezi Mungu basi watampenda wakazi wa mbinguni na ardhini, na atakayemchukia Mwenyezi Mungu watamchukia wakazi wa mbinguni na ardhini.
- Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na atawekewa kukubalika katika Ardhi", si lazima wamkubali watu wote, bali ni kwa kiwango alichokitaka Mwenyezi Mungu kwake cha kukubalika katika Ardhi, ndivyo hivyo kwa sababu uadui wa watu waovu kwa watu wema unafahamika.
- Himizo la kutimiza amali za wema kwa namna zake tofauti tofauti, za faradhi za sunna, na tahadhari ya maasi na uzushi; kwa sababu ndio huchukuliwa kama sababu ya kupata hasira.
- Amesema bin Hajari: Na inachukuliwa hapa kuwa mapenzi ya nyoyo za watu ni alama ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na inaungwa mkono na hadithi ya jeneza, aliyosema Mtume: "Nyinyi ndio mashahidi wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi".
- Amesema binil Arabi Al-Maaliki: Na inakusudiwa wakazi wa ardhi wale wanaomfahamu pasina wasiomfahamu wala kuwahi kumsikia.
صحيح البخاري (4/ 111) (3209). صحيح مسلم (4/ 2030) (2637). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 268). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 355). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 308). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 455).