Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" Yaani: Ninashikamana na kuegemea kwa Mwenyezi Mungu na sifa zake. "Na kwa uso wake Mkarimu" Yaani: Mkarim mtoaji, "Na kwa mamlaka yake) Yaani: Ushindi wake na uweza wake kwa amtakaye katika viumbe wake "Wa tangu" Yaani: Wa zamani na wa milele. "Kutokana na Shetani aliyelaaniwa" Yaani: Aliyetengwa na kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, yaani: Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi kutokana na wasi wasi wake na upotoshaji wake na hatua zake na hatari zake, na udanganyifu wake na upotoshaji wake, kwani yeye ndiye sababu ya upotofu, na ndio mchochezi wa upotofu na ujinga, akaulizwa Abdillah bin Amri "Hivyo tu" Yaani: Je, alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni hivyo tu? Akasema: Ndio. Atakaposema dua hii mwenye kuingia msikitini; Shetani husema: Muingiaji kaihifadhi nafsi yake dhidi yangu wakati wake wote, mchana wake na usiku wake.
- Fadhila za kuomba kwa dua hii wakati wa kuingia msikitini, nakuwa dua hii humkinga msemaji wake kutokana na Shetani siku nzima.
- Tahadhari kutokana na Shetani, nakuwa humuwinda Muislamu; kwa ajili ya kumpoteza na kumshawishi.
- Mtu atalindwa kutokana na upotofu na udanganyifu wa Shetani kwa kiwango ambacho moyo wake unamwamini Mwenyezi Mungu na kuihudhurisha dua hii, na kuamini kwake ahadi za Mwenyezi Mungu zinazotokana nayo.
سنن أبي داود (1/ 349) (466). شرح سنن أبي داود، لبدر الدين العيني (2/ 374). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 627).