Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku

عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ، يَقُولُ: «مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ؟ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ؟ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ؟».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, husema: "Ni nani anayeniomba nimjibu? Ni nani anayenitaka shida yake nimpe? Ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe?".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, na anawahamasisha waja wake wamuombe, kwani yeye anamjibu mwenye kumuomba, na anawahimiza wamtake haja zao, kwani yeye humpa anayemuomba, na anawaita wamuombe msamaha kutokana na madhambi yao kwani yeye huwasamehe waja wake waumini.

Mafunzo
  1. Ubora wa theluthi ya mwisho ya usiku na swala na dua na kutaka msamaha ndani yake.
  2. Ni wajibu kwa mwanadamu wakati wa kusikia hadithi hii awe na pupa kubwa ya kunufaika na nyakati za kujibiwa dua.
Marejeo

صحيح البخاري صحيح البخاري (2/ 53) (1145). صحيح مسلم (1/ 521) (758). الإفصاح عن معاني الصحاح، ليحيى بن هبيرة (6/ 195).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com