Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".
Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineoDarajaAmesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.

Mafunzo
  1. Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upole wake kwa waja wake kiasi ambacho amewaondolea madhambi pale yatakapojitokeza maasi katika hali hizi tatu.
  2. Fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya umma wake.
  3. Kuondolewa dhambi haimaanishi kuondolewa hukumu au dhamana, mfano atakayesahau udhu, na akaswali kwa kudhani kuwa yuko twahara, hana dhambi katika hilo, lakini atatakiwa kutia udhu na kurudia swala.
  4. Lazima katika kuondolewa dhambi kwa kulazimishwa kuwe na sharti, mfano kama akiwa mlazimishaji anauwezo wa kutimiza alichotishia.
Marejeo

الأربعون النووية (ص127) (ح39). سنن ابن ماجه (3/ 200) (2045). السنن الكبرى للبيهقي (7/ 584) (15094). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص89). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص382).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com