Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kumpwekesha Allah kwa vitendo vyake (Uumbaji)

Hadithi 7

Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa

عن أبي ذر الغفاري رضي الله عنه مرفوعاً: "ما الكرسي في العرش إلا كحلقة من حديد ألقيت بين ظهري فلاة من الأرض".
Kutoka kwa Abuu Dharri Al-Ghifaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa pana".
Imepokelewa na Abii Shayba katika kitabuchake Al Arshi - Imepokelewa na Adh-dhahaby katika kitabu cha UluwwiDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ya Abuu dharri kuwa kursiy pamoja na upana wake na ukubwa wake ukilinganisha na Arshi ni kama bangili la chuma lililowekwa katika jangwa la ardhi pana; Na hii inaonyesha ukubwa na utukufu wa muumbaji wake na uwezo wake uliotimia.

Marejeo

1- فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، مطبعة السنة المحمدية، القاهرة، مصر، الطبعة: السابعة، 1377هـ - 1957م. 2- القول المفيد على كتاب التوحيد، دار ابن الجوزي، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الثانية, محرم، 1424ه. 3- الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ- 2001م. 4- الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م. 5- التمهيد لشرح كتاب التوحيد، دار التوحيد، تاريخ النشر: 1424هـ. 6- شرح العقيدة الطحاوية، المؤلف: محمد ناصر الدين الألباني، الناشر: المكتب الإسلامي – بيروت الطبعة: الثانية، - 1414ه. 7- العرش وما روي فيه، المؤلف: محمد بن عثمان ابن أبي شيبة العبسي، تحقيق: محمد بن حمد الحمود، الناشر: مكتبة المعلا – الكويت، الطبعة الأولى، 1406ه.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قال: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الذَّنْبِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللهِ؟ قَالَ: «أَنْ تَجْعَلَ لِلهِ نِدًّا وَهُوَ خَلَقَكَ» قُلْتُ: إِنَّ ذَلِكَ لَعَظِيمٌ، قُلْتُ: ثُمَّ أَيُّ؟ قَالَ: «وَأَنْ تَقْتُلَ وَلَدَكَ؛ تَخَافُ أَنْ يَطْعَمَ مَعَكَ» قُلْتُ: ثُمَّ أَيُّ؟ قَالَ: «أَنْ تُزَانِيَ حَلِيلَةَ جَارِكَ».
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba" Nikasema: Hakika hilo ni jambo kubwa, nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Na kumuua mwanao; ukiogopea atakula pamoja nawe" Nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Ni wewe kumzini mke wa jirani yako".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu dhambi kubwa akasema: Kubwa zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mfano katika uungu wake au uumbaji wake au majina yake na sifa zake, na dhambi hili halisamehe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa toba, na akifa mfanyaji wake huyo atakaa milele motoni. Kisha ni mtu kumuua mwanaye kwa kuchelea kula naye, na kuua nafsi ni haramu, lakini dhambi linakuwa kubwa pale anapokuwa muuliwaji ni ndugu wa damu wa muuaji, na dhambi lake linakuwa kubwa pia pale linapokuwa lengo la muuaji ni kuchelea kushirikiana pamoja na muuliwaji katika riziki ya Mwenyezi Mungu. Kisha ni mtu kumzini mke wa jirani yake kwa kujaribu kumhadaa mke wa jirani yake mpaka akafikia kuzini naye, naye akamkubalia, Na zinaa ni haramu lakini dhambi lake linakuwa kubwa anapokuwa mziniwa ni mke wa jirani ambaye sheria imeusia kumtendea wema na kuishi naye vizuri.

Mafunzo
  1. Kutofautiana ukubwa kwa madhambi, kama ambavyo matendo mema yanazidiana katika ubora.
  2. Dhambi kubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha kumuua mtoto kwa kuchelea kula naye, kisha kumzini mke wa jirani yako.
  3. Riziki iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na amechukua jukumu -Aliyetakasika- la kuwaruzuku viumbe.
  4. Ukubwa wa haki ya jirani, nakuwa kumuudhi ni dhambi kubwa kuliko kumuudhi mwingine.
  5. Muumba ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa yeye peke yake asiye na mshirika wake.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 18) (4477). صحيح مسلم (1/ 90) (86). شرح النووي على مسلم (2/ 79). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 288). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 335).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ: دَخَلَ عَلَيَّ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَدْ سَتَرْتُ سَهْوَةً لِي بِقِرَامٍ فِيهِ تَمَاثِيلُ، فَلَمَّا رَآهُ هَتَكَهُ وَتَلَوَّنَ وَجْهُهُ وَقَالَ: «يَا عَائِشَةُ، أَشَدُّ النَّاسِ عَذَابًا عِنْدَ اللهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ اللهِ» قَالَتْ عَائِشَةُ: «فَقَطَعْنَاهُ فَجَعَلْنَا مِنْهُ وِسَادَةً أَوْ وِسَادَتَيْنِ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka pazia lenye picha kwa kusahau, alipoliona akalichana na akaghadhibika mpaka uso wake ukabadilika rangi, na akasema: "Ewe Aisha, Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu" Aisha anasema: "Tukalichana vipande vipande vingine tukavifanya kuwa mto au mito miwili ya kulalia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhiwa humo bidhaa kwa kitambaa ambacho kina picha za viumbe hai, ikabadilika rangi ya uso wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akalifunua, na akasema: Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Kiyama ni wale wenye kufanya mfano kwa kutengeneza picha za vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu. Aisha akasema: Tukakifanya kitambaa kile kuwa ni mto mmoja au miwili.

Mafunzo
  1. Kukemea uovu wakati wa kuuona na kutochelewa katika hilo, madam hakuna madhara makubwa katika hilo.
  2. Adhabu siku ya Kiyama itatofautiana kulingana na ukubwa wa dhambi.
  3. Kupiga picha za viumbe hai ni katika madhambi makubwa.
  4. Miongoni mwa hekima za kuharamishwa kupiga picha za viumbe hai ni kufafanisha vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu, sawa sawa mpigaji awe kakusudia kufananisha au hakukusudia hivyo.
  5. Sheria imetilia umuhimu juu ya kuhifadhi mali kwa kuitumia katika matumizi mengine baada ya kuitoa katika matumizi ya haram.
  6. Katazo la kutengeneza picha za viumbe hai kwa umbile lolote lile litakalokuwa, hata kama litakuwa ni dhalili.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 168) (5954). صحيح مسلم (3/ 1668) (2107). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 442). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص399). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص441). كتاب التوحيد لمحمد بن عبد الوهاب (ص138).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto

عن أنس بن مالك رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمُعَاذٌ رَدِيفُهُ عَلَى الرَّحْلِ قَالَ: «يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، قَالَ: «يَا مُعَاذُ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، ثَلَاثًا، قَالَ: «مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللهُ عَلَى النَّارِ»، قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَفَلَا أُخْبِرُ بِهِ النَّاسَ فَيَسْتَبْشِرُوا؟ قَالَ: «إِذًا يَتَّكِلُوا». وَأَخْبَرَ بِهَا مُعَاذٌ عِنْدَ مَوْتِهِ تَأَثُّمًا.
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto", akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je, niwaeleze watu ili wapate habari njema? Akasema: "Ukifanya hivyo, watabweteka". Na alieleza Muadhi jambo hili wakati wa kifo chake kwa kuogopa kupata dhambi za kuficha elimu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Muadhi bin Jabali -Radhi za Allah ziwe juu yake- amepanda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya mnyama wake, akamuita: Ewe Muadhi? Akarudia wito mara tatu; Kwa kusisitiza umuhimu wa yale atakayomueleza. Na mara zote hizo Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akimjibu kwa kusema: "Labaika kwa heshima yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Yaani: Nimekujibu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jibu moja moja, na ninataka utukufu kwa kukujibu wewe. Akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hakuna yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuaubudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isopokuwa Allah, na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa ukweli toka moyoni mwake, si muongo, ikiwa atakufa katika hali hii basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni. Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- awaeleze watu ili wafurahi na wajipe bishara njema? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akachelea watu kubweteka katika hilo, na wapunguze kufanya matendo. Muadhi hakumsimulia hilo yeyote ila kabla ya kifo chake; kwa kuhofia kuingia katika dhambi za kuficha elimu.

Mafunzo
  1. Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumpakiza kwake Muadhi nyuma ya mnyama wake.
  2. Njia ya ufundishaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba alirudia rudia wito kwa Muadhi ili akaze usikivu wake kwa yale atayoyazungumza.
  3. Katika sharti za shahada: Ya Kushuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni awe msemaji wake ni mkweli na yakini, asiwe muongo au na shaka.
  4. Watu wa tauhidi hawatokaa milele katika moto wa Jahannam, hata kama watauingia kwa sababu ya madhambi yao; watatolewa baada ya kusafishwa.
  5. Fadhila za shahada mbili kwa atakayezisema akiwa mkweli.
  6. Kufaa kuacha kuzungumza baadhi ya mazungumzo katika baadhi ya hali, yatakapoambatana na madhara.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 37) (128). صحيح مسلم (1/ 61) (32). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 377). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 487). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 496).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

"Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,

Mafunzo
  1. Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
  2. Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
  3. Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
  4. Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
  5. Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 169) (846)، صحيح مسلم (1/ 83) (71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 484)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 260).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?

عَنْ ‌قَتَادَةَ رحمه الله قال: حَدَّثَنَا ‌أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا نَبِيَّ اللهِ كَيْفَ يُحْشَرُ الْكَافِرُ عَلَى وَجْهِهِ؟ قَالَ: «أَلَيْسَ الَّذِي أَمْشَاهُ عَلَى الرِّجْلَيْنِ فِي الدُّنْيَا قَادِرًا عَلَى أَنْ يُمْشِيَهُ عَلَى وَجْهِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ؟» قَالَ قَتَادَةُ: بَلَى وَعِزَّةِ رَبِّنَا.
Imepokelewa kutoka kwa Qatadah -Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Alitusimulia Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi kafiri atafufuliwa akitembea kwa uso wake? Akasema: "Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?" Akasema Qatadah: Kwa nini asiweze, ninaapa kwa utukufu wa Mola wetu anaweza kufanya hivyo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vipi atafufuliwa Kafiri akitembea kwa uso wake siku ya Kiyama? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Hivi Mwenyezi Mungu aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hapa Duniani hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?! Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.

Mafunzo
  1. Udhalili utampata Kafiri siku ya Kiyama na atatembea kwa uso wake.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 109) (6523)، صحيح مسلم (4/ 2161) (2806)، الإفصاح عن معاني الصحاح (5/200)، فتح الباري (11/382)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (23/ 105)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (43/ 454).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: Muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapo omba basi muombe Mwenyezi Mungu, na ukitaka msaada muombe msaada Mwenyezi Mungu

عَنْ أَبِي العَبَّاسِ، عَبْدِ الله بْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: كُنْت خَلْفَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا، فَقَالَ: «يَا غُلَامِ! إنِّي أُعَلِّمُك كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللَّهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ الله تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلِ اللهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاَللهِ، وَاعْلَمْ أَنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ، وَإِنِ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ؛ رُفِعَتِ الأَقْلَامُ، وَجَفَّتِ الصُّحُفُ». وَفِي رِوَايَةِ غَيْرِ التِّرْمِذِيِّ: «احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعَرَّفْ إلَى اللهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ أَنَّ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ، وَمَا أَصَابَك لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ أَنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنْ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا».
Kutoka kwa Abul-Abbas, Abdallah bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: Muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapo omba basi muombe Mwenyezi Mungu, na ukitaka msaada muombe msaada Mwenyezi Mungu, na tambua: kuwa laiti watu wote wangelikusanyika ili wakunufaishe wewe kwa kitu chochote, hawatoweza kukunufaisha isipokuwa kwa kitu ambacho tayari kakiandika Mwenyezi Mungu kwako, na ikiwa watakusanyika kwa ajili ya kukudhuru wewe kwa kitu chochote, hawatoweza kukudhuru kwa kitu chochote isipokuwa kile ambacho kakuandikia Mwenyezi Mungu kikupate, kalamu zimenyanyuliwa na kurasa zimekauka" Na katika riwaya isiyokuwa ya Tirmidhi: "Muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, Jipendekeze kwa Mwenyezi Mungu wakati wa raha atakujua wakati wa shida, na tambua kuwa yaliyo kukosa hayakua ni yenye kukupata, na yaliyo kupata hayakuwa ni yenye kukukosa, na tambua kuwa msada huambatana na subira, na kuwa faraja huwa pamoja na matatizo, na kuwa uzito huwa pamoja na wepesi".
Imepokelewa naTirmidhiy na wengineoDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa yeye alipokuwa kijana mdogo alikuwa kapanda pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema kumwambia -Amani iwe juu yake-: Hakika mimi ninakufundisha vitu na mambo ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kwayo: Muhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi maamrisho yake na kuepuka makatazo yake, kiasi kwamba akukute katika utiifu na yale yenye kukuweka karibu naye, na asikukute katika maasi na madhambi, ikiwa utafanya hivyo basi malipo yako yatakuwa ni Mwenyezi Mungu kukuhifadhi kutokana na kero za Dunia na Akhera, na atakunusuru katika mambo yako magumu mahala popote utakapoelekea. Na ukitaka kuomba jambo, basi usimuombe ila Mwenyezi Mungu kwani Yeye pekee ndiye mwenye kuwajibu waombaji. Na ukitaka msaada basi usiutake ila kwa Mwenyezi Mungu. Na uwe na yakini kuwa hutopata manufaa yoyote hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukunufaisha, isipokuwa kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu kwako, na wala hutopata madhara hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukudhuru, isipokuwa kwa lile alilolikadiria Mwenyezi Mungu juu yako. Na kuwa jambo hili kashaliandika Mwenyezi Mungu Mtukufu na akalikadiria kulingana na namna hekima na elimu yake zilivyopelekea, na hakuna kubadilishwa yale aliyoyaandika Mwenyezi Mungu. Na kwamba atakayemuhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi amri zake na kuyaepuka makatazo yake; basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa mbele ya mja kwa kuyajua matatizo yatakayomfika na atamnusuru na kumpa msaada. Na kwamba mwanadamu atakapomtii Mwenyezi Mungu wakati wa raha basi Mwenyezi Mungu atamletea faraja na njia ya kutokea wakati wa shida, hivyo na aridhie kila mja na kile alichokikadiria Mwenyezi Mungu cha kheri na shari. Na kukiwa na matatizo na mitihani basi mja ashikamane na subira kwani subira ni ufunguo wa faraja, na kwamba mitihani ikizidi kuwa mingi ndio faraja huja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba uzito unapotokea Mwenyezi Mungu huufuatisha na wepesi.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kuwafundisha vijana na watoto wadogo mambo ya dini kuanzia Tauhidi na adabu na mengineyo.
  2. Malipo huenda sawa na matendo.
  3. Amri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kutawakali kwake bila kumtegemea asiyekuwa yeye, na yeye ndiye msaidizi bora.
  4. Kuamini maamuzi na mipango ya Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo, nakuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kila kitu.
  5. Atakayetelekeza amri ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu naye humtelekeza na humnyima ulinzi.
  6. Habari njema kubwa kwa mwanadamu kuwa pale unapompata uzito basi asubiri wepesi.
  7. Kuliwazwa mja pale inapotokea mitihani, na kuyakosa yale ayapendayo, kwa mujibu wa kauli yake: "Na tambua kuwa yaliyokufika hayakuwa ni yenye kukukosa, na yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata" Sentensi ya kwanza ni kuliwazwa wakati wa kufikwa na yenye kuchukiza, na ya pili ni katika kuyakosa yale yenye kupendeka.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 284) (2516). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص42). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص200). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص69).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com