Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa umma kabla yake isipokuwa huwa na watu safi na watetezi, na mujahidina wa kweli kutoka katika umma wake wanaofaa kwa ukhalifa (uongozi) baada yake, wanaofuata Sunna zake na kufuata amri yake, kisha baada ya hao watangulizi wema wanakuja watu ambao hawana kheri ndani yake; Wanasema wasiyoyafanya, na wanafanya yale ambayo hawakuamrishwa kuyafanya, na atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ni Muumini, atakayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumini, na hakuna imani hata chembe ya haradali (ulezi) baada yake.
- Himizo la kupambana na wanaokwenda kinyume na sheria kwa kauli zao na vitendo vyao.
- Moyo kutokukemea uovu ni dalili ya udhaifu wa imani au kutoweka kwake.
- Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwafanyia wepesi Manabii kuwapata wenye kubeba ujumbe wao baada yao.
- Atakayetaka kusalimika basi anatakiwa kufuata njia ya Manabii; kwa sababu kila njia isiyokuwa njia yao ni maangamivu na upotovu.
- Kila zama zinavyozidi kuwa mbali na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Masahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao watu huzidi kuacha mafundisho na kufuata matamanio na kuzusha mambo ya uzushi.
- Kumebainishwa daraja za Jihadi, nakuwa ni kwa mkono kwa mwenye kuweza kuuondoa uovu, kama wasimamizi na viongozi na watawala, na kwa kauli inakuwa kwa kubainisha haki na kuwalingania watu, na kwa moyo inakuwa kwa kuukemea uovu na kutoupenda au kuuridhia.
- Ulazima wa kuamrisha mema na kukataza uovu.
صحيح مسلم (1/ 69) (50). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 276). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص148). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 16). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 209).