Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسَ الْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ وَلاَ اللَّعَّانِ وَلاَ الفَاحِشِ وَلاَ البَذِيءِ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa si katika mambo ya muumini mwenye imani kamili kuwa mtoa aibu za watu katika nasaba zao, wala mwingi wa matusi na laana, wala muovu wa vitendo na kauli ambaye hana haya.

Mafunzo
  1. Kukanushwa imani katika dalili za kisheria hakuwi isipokuwa kwa kutenda kitendo cha haram au kuacha wajibu.
  2. Himizo la kuhifadhi viungo na kuvilinda na mabaya, hasa hasa ulimi.
  3. Amesema As-Sanadi: Na katika tamko la kusisitiza katika kauli yake (Mwingi kutukana, na mwingi wa kutoa laana) Ni dalili kuwa kutoa matusi na laana mara chache si vibaya kwa mtu atakayestahiki hilo, na wala haidhuru mtu kusifika kwa sifa za waumini.
Marejeo

سنن الترمذي (3/ 520) (1977)، تحفة الأحوذي (6/ 95)، مجموع الفتاوى (12/ 478).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com