Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ مَكَارِمَ الْأَخْلَاقِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema"
Imepokelewa na Al-Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Ahmad na Al-BayhaqiDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alimtuma yeye ili akamilishe mambo bora na tabia zilizo njema; kiasi kwamba alitumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili atimize yale waliyokuwa nayo Mitume, na alikuja kukamilisha tabia njema za waarabu, kwani walikuwa wakipenda kutenda kheri na wakichukia shari, walikuwa ni watu wenye utu na ukarimu na utukufu; akatumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili kukamilishe mapungufu yaliyoko katika tabia zao, kama kujifaharisha kwao kwa nasaba, na kujikweza na kumdharau fakiri na nyinginezo.

Mafunzo
  1. Himizo la kuwa na tabia njema, na katazo la kinyume chake.
  2. Kumebainishwa umuhimu wa tabia njema katika sheria ya Uislamu na kwamba ni katika vipaumbele vyake.
  3. Watu wa zama za ujinga walikuwa na mabaki ya tabia njema, ikiwemo ukarimu na ushujaa na mengineyo, Uislamu ukaja kuyakamilisha.
Marejeo

الأدب المفرد (ص104) (273). مسند أحمد (14/ 512) (8952). السنن الكبرى للبيهقي (10/ 191) (20819). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (22/ 118).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com