Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote

عَنْ جَرِيرٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ يُحْرَمِ الرِّفْقَ يُحْرَمِ الْخَيْرَ».
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunyimwa upole akawa hakuafikishwa katika mambo ya dini na dunia, na katika mambo yake mwenyewe, na yale anayoyafanya na wengine, basi atakuwa kanyimwa kheri yote.

Mafunzo
  1. Fadhila za upole na himizo la kujipamba na tabia hiyo, na kemeo la ukali.
  2. Upole hunyoosha kheri za Dunia na Akhera na hupanua mlango wa baraka, lakini ukali ni kinyume chake.
  3. Upole ni taji ambalo hutokana na tabia njema na amani, na jeuri hutokana na hasira na ufidhuli, ndio maana aliusifia sana upole Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapitiliza katika kusifu.
  4. Alisema Sufian Al-Thauri Mwenyezi Mungu amrehemu, akiwaambia jamaa zake: Je, mnajua upole ni nini? Ni kuweka mambo mahali pake panapofaa, na ukali mahali pake panapofaa, na upole mahali pake panapofaa, upanga mahali pake panapofaa, na mjeledi mahali pake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2003) (2592). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 532). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص416). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 592). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (9/ 152). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 687). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (6/ 241).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com