Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu
عن سعد بن أبي وقاص رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْعَبْدَ التَّقِيَّ الْغَنِيَّ الْخَفِيَّ».
Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake,
Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake.
Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine.
Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.
Mafunzo
Zimebainishwa baadhi ya sifa zinazopelekea mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, nazo ni uchamungu na unyenyekevu na kuridhika na yale aliyoyagawa Mwenyezi Mungu.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2277) (2965).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 651).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 509).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 509).
شرح النووي على مسلم (18/ 100).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com