Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii

عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ لَا يَرْحَمِ النَّاسَ لَا يَرْحَمْهُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ».
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii, huruma ya mja kwa viumbe ni katika sababu kubwa za kupata huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo
  1. Huruma inahitajika kwa viumbe wote, lakini wametajwa watu kama sehemu ya kuwapa kipaumbele.
  2. Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa huruma na anawahurumia waja wake wenye huruma, kwani malipo huendana na matendo.
  3. Huruma kwa watu inakusanya kuwafikishia kheri na kuwazuilia shari na kuamiliana nao kwa wema.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 10) (6013). صحيح مسلم (4/ 1809) (2319). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 553). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 247). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 319).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com